" REA YAENDELEA NA UHAMASISHAJI WA NISHATI VIJIJINI MARA

REA YAENDELEA NA UHAMASISHAJI WA NISHATI VIJIJINI MARA







📌 *Wananchi wahamasika kujiunga na huduma ya umeme* .


📌 *Wananchi waunga mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia* .


📍 *Mara* 


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na ziara ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Mara.


Uhamasishaji umehusisha utoaji wa elimu kwa wananachi namna ya kufanya maombi ya kujiunga na huduma ya umeme huku lengo kuu likiwa ni  kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 


Aidha, Wakala umefanya Kampeni zinahusisha utoaji wa elimu kuhusu umuhimu na faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utunzaji wa afya, mazingira pamoja na usawa wa kijinsia.


 Aidha, Wakala umetoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi bora  ya umeme hususani katika shughuli za uzalishaji ikiwemo shughuli za biashara, kilimo, na shughuli za nyumbani.


Vile vile, Wakala umetoa elimu kuhusu taratibu rahisi za kuomba umeme, Kufundisha umuhimu wa usalama wakati wa matumizi ya umeme, utunzaji wa miundombinu ya umeme na Kuhimiza wananchi kushirikiana na serikali , REA na mkandarasi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.


Uhamasishaji huu ni sehemu ya jitihada za serikali za kuboresha maisha ya wananchi vijijini kwa kutoa nishati bora na ya kuaminika.


 *Mwisho* .

Post a Comment

Previous Post Next Post