Rai hiyo imetolewa leo Februari 27, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Magu,Jubilate Lawuo wakati akifungua maadhimisho,Elimu na uzinduzi wa mitambo katika teknolojia ya ukandarasi wa madini ambapo madhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Nyamhongolo jijini mwanza.
Lawuo amesema mikopo ya Halmashauri inasaidia sana vijana katika kujiajiri kwa mtu mmoja , mmoja au vikundi.
" Serikali yetu imeweka mazingira mazuri kwa vijana wetu kukopeshwa kupitia vikundi vyao. Pia na Halmashauri zetu zinajitaid sana katika kusaidia vijana wetu" alisema.
Vile vile, Lawuo ameagiza vijana waweze kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya wakandarasi ili waweze kuona mitambo mbalimbali ya uchimbaji na ukandarasi inayopatikana.
Ameongeza kuwa mkoa wa Mwanza katika wilaya za Kwimba na Sengerema kuna migodi mbalimbali iliyoajiri vijana wa kitanzania wanaojihusisha na uchimbaji wa madini.
Naye Mwenyekiti wa maonyesho ya wakandarasi na wachimbaji, George Mandia alisema maonyesho yao ni endelevu karibia kila mwezi yatakuwa yakifanyikia mikoa tofauti.
Mandia ameeleza maonyesho mwezi Machi yatafanyika mkoani Arusha, Aprili maonyesho yatakuwa mkoani Geita na Mei yatakuwa mkoa wa Simiyu.
Ameshukuru chuo cha ufundi nchini(VETA) tawi la Mwanza kwa kuzalisha wahandisi na mafundi mbalimbali ambapo wamekuwa wakisaidia sana katika shughuli za uchimbaji.
Kwa upande wake injinia Benadi ambaye pia ni mratibu wa maonyesho hayo ameipongeza ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano waliouwonesha katika kufanikisha maonesho mkoani hapa .
Ikumbukwe kuwaa maonesho hayo yanabebwa na Kauli mbiu inayosema mwendelezo wa uhandisi na ukandarasi kimaendeleo.
























Post a Comment