" Amdunga Mchumba Wake Sindano Yenye HIV Kisa Kukataa Kuoana

Amdunga Mchumba Wake Sindano Yenye HIV Kisa Kukataa Kuoana

 

Amdunga Mchumba Wake Sindano Yenye HIV Kisa Kukataa Kuoana
Amdunga Mchumba Wake Sindano Yenye HIV Kisa Kukataa Kuoana

TUKIO la kushangaza limetokea jimbo la Telangana nchini India, baada ya mwanaume mmoja aliyekuwa amejawa na hasira kumdunga sindano iliyo na damu yenye virusi vya HIV mwanamke mmoja aliyekataa kuoleka na yeye.

Wazazi wa msichana huyo wanasema tukio hilo lilitokea Machi 11, mwaka huu. Huku polisi wakisema mwanamke huyo kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini.

Kwa mujibu wa polisi miezi michache iliyopita, familia ya mwanamke wa miaka 24 wanaoishi eneo la Annojiguda nje ya mji wa Hyderabad, na familia moja ya kijana mwenye umri wa miaka 25 ambao walikuwa majirani, walikuwa wamekubali kuwaoza wawili hao.

Mshukiwa alikuwa akiishi na Mama yake baada ya kifo cha Baba yake. na kwamba kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya uchukuzi.

“Kwasababu wazazi wa mshukiwa walikuwa wakishukiwa kuwa na virusi vya HIV, wazazi wa msichana walitaka kijana huyo kupimwa kwanza kabla ya harusi kufanyika.

“Ukaguzi wa maabara ulibaini kwamba kijana huyo ana virusi vya HIV. Harusi hiyo ilisimamishwa,” hii ni kulingana na ripoti iliyoandikiwa na familia ya msichana katika kituo cha polisi.

Ofisa mmoja katika kituo cha polisi cha Pocharam alisema “Kijana huyo alikasirika baada ya harusi hiyo kusitishwa.”

“Uchunguzi wetu umebaini kijana huyu alimdunga msichana huyo na sindano, ili kubadilishana damu yake iwe ya msichana huyo pia. Akidhani akimdunga na virusi vya HIV hataweza kuoleka na mtu mwingine,” alisema polisi huyo.

“Alijua msichana wetu yuko nyumbani pekee yake. Aliingia kwenye nyumba na kumpa posa nyingine, alipokataa alimdunga sindano iliyokuwa na damu kwa nguvu,” wazazi wa msichana walisema.

Pia ilielezwa kuwa msichana huyo alikuwa amejawa na wasiwasi kuhusu tukio hilo kwa hivyo hakuripoti kwa wazazi wake.

Siku chache baadaye, alianza kuhisi na joto jingi na mwili kuuma, wazazi wake walimpeleka hospitalini, alipoulizwa maswali na daktari alisimulia kilichotokea.

“Kijana huyo alitaka kumuua msichana wetu kwa kumdunga na virusi vya HIV. Sheria kali dhidi yake inapaswa kuchukuliwa,” wazazi wa msichana huyo walisema.

Polisi wa upelelezi Vijay Bhaskar Reddy alieleza kuwa walipokea kesi hiyo Machi 13. Na mshukiwa alikamatwa.

“Tunachunguza kujua alipataje virusi vya HIV. Mara anasema alizaliwa navyo, mara anasema aliambukizwa, tunachunguza suala hilo,” walisema polisi.

Mwanamke aliyeathirika sasa anapokea matibabu. Kulingana na polisi, vipimo vya damu vya msichana huyo kwa sasa vinaonyesha hajapata virusi vya HIV, ila uchunguzi zaidi bado unafanyika.

Kulingana na madaktari uhakika zaidi utapatikana baada ya miezi miwili.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post