Serikali imepiga hatua kubwa katika kuimarisha sekta ya uvuvi na usafirishaji wa mizigo maalum nchini.
Mradi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko, unaotekelezwa kwa ufadhili wa asilimia 100 wa serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 280, umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake hadi tarehe 21 Machi 2026.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa serikali, Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari South Port, Mwanza amefafanua kuwa gati lenye urefu wa mita 315 limekamilika kwa asilimia 100, na mradi huu unatarajiwa kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la taifa pamoja na kuzalisha ajira zaidi ya 1,000.
“ Mradi huu pia utasaidia kupata fedha za kigeni kupitia usindikaji na mauzo ya samaki nje ya nchi” alisema Msigwa.
Akizungumzia zaidi bandari hiyo ya Uvuvi ya Kilwa Masoko hadi kufikia tarehe 21 Machi 2026, ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 315 umekamilika kwa asilimia 100 huku ujenzi wa miundombinu ya huduma pamoja na mitambo ukiwa umefikia asilimia 98 na ujenzi wa jengo la kupokelea pamoja na soko la kunadi samaki umefikia asilimia 91.
Kukamilika kwa bandari hii kunatarajiwa kuleta manufaa makubwa kiuchumi na Kijamii yakiwemo; Kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la taifa, kuongeza ajira, ambapo tayari zaidi ya ajira 1,000 zimetolewa wakati wa ujenzi. Kukuza uchumi kupitia upatikanaji wa fedha za kigeni, kutokana na usindikaji wa samaki kwa soko la ndani na mauzo ya nje. Kwa ujumla, Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko ni mradi muhimu wa kimkakati unaolenga kuimarisha sekta ya uvuvi na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Sambamba na mafanikio ya uvuvi, serikali pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa gati jipya na mfumo wa 'conveyor belt' katika Bandari ya Kisiwa Mgao mkoani Mtwara kwa ajili ya mizigo michafu kama makaa ya mawe na saruji.
Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 434.53, ambapo hadi Februari 2026 jumla ya shilingi bilioni 128.20 tayari zimetumika kumlipa mkandarasi.
Hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 33, na ukikamilika utachochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya usafirishaji na biashara.
Ujenzi wa bandari hiyo ni sehemu ya uwekezaji wa zaidi ya shilingi trilioni moja katika sekta ya uchukuzi zinazoonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha uchumi wa bluu na miundombinu ya kimkakati.
mwisho
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment