" Benki ya TADB yakabidhi hundi BIL 7 kwa Serikali mradi wa BBT Uvuvi

Benki ya TADB yakabidhi hundi BIL 7 kwa Serikali mradi wa BBT Uvuvi

 Baraka Kifumbe MwanzaBenki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 7 kwa ajili ya kuwawezesha vijana waliohitimu programu ya BBT–Uvuvi, kusaidia utekelezaji wa awamu ya pili ya miradi ya uvuvi inayofanywa na vijana hao katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.Katika awamu ya kwanza ya mradi huu, TADB imetoa jumla ya TZS Bilioni 14.07 kwa wanufaika zaidi ya 1,300 wanaojihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, kati yao vijana ni 577, sawa na 44%.Hundi ya fedha TZS Billion 7 imekabidhiwa na Mhe. Dkt. Joel Nanauka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, kwa niaba ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kukabidhi mitaji ya kuwezesha utekelezaji wa miradi iliyoibuliwa na vijana wa BBT–Uvuvi iliyofanyika katika chuo Uvuvi Mwanza (FETA).Kupitia uwezeshaji wa mradi huo, vijana wa BBT–Uvuvi watajishughulisha na ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (cage fish farming) katika maji ya asili ya ziwa Viktoria. Mbinu hii ya kisasa inalenga kuongeza uzalishaji wa samaki, kuboresha kipato cha vijana na kuimarisha mchango wa sekta ya uvuvi katika uchumi wa taifa.Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Dkt. Nanauka alieleza kuwa uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya Serikali ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta yenye fursa kubwa kama uvuvi.Kwa upande wake, Mhe. Ng’wasi Kamani, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, alisema kuwa mradi huo ni awamu ya pili na hatua muhimu katika kuendeleza sekta ya uvuvi nchini kupitia matumizi ya teknolojia na mbinu za kisasa. Alieleza kuwa matumizi ya vizimba vya kufugia samaki yataongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji na ubora wa samaki, pamoja na kusaidia kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Mkani Waziri,  ameeleza kuwa uwezeshaji huo ni sehemu ya dhamira ya benki ya kuimarisha upatikanaji wa mitaji katika sekta za kilimo ikiwemo uvuvi, kwa lengo la kuongeza uzalishaji, kukuza ajira kwa vijana na wanawake na kuimarisha usalama wa chakula nchini.Programu ya BBT–Uvuvi ni sehemu ya mpango wa Building a Better Tomorrow (BBT) unaotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kuanzisha na kuendeleza miradi ya uzalishaji mali katika sekta mbalimbali za uchumi.Kupitia miradi hiyo, vijana wanatarajiwa kuongeza uzalishaji wa samaki, kuboreHafla hiyo ya uzinduzi wa kukabidhi mitaji ya kuwezesha utekelezaji wa miradi iliyobuniwa na vijana wa BBT Uvuvi ilifanyika katika viwanja vya chuo cha FETA Jijini Mwanza.

  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


 

Post a Comment

Previous Post Next Post