" RAIS RUTO: USTAWI, AMANI NA MSHIKAMANO IMEKUWA DIRA

RAIS RUTO: USTAWI, AMANI NA MSHIKAMANO IMEKUWA DIRA

Na, Egidia Vedasto,

Misalaba Media, Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Kenya  na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki William Ruto akitoa hotuba yake  katika mkutano wa jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha amesisitiza ustawi, amani na mshikamano kama dira iliyostawisha jumuiya hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi uenyekiti amesema  kuwa amani na utulivu wa kikanda ni msingi muhimu wa ustawi wa pamoja, ujumuishaji wa  kiuchumi, amani na usalama, maendeleo ya miundo mbinu na ushirikiano unaolenga wananchi.

Aidha Rais Ruto amesisitiza kuweka mkazo katika usalama wa chakula, kukabiliana na athari za za mabadiliko ya tabia ya nchi na maendeleo endelevu.

Rais Ruto amesisitiza ajenda ya Jumuiya iendelee kuzingatia kuboresha maisha ya wananchi, kupitia ajira, elimu bora,hususan za afya zilizoimarishwa na uhuru zaidi wa watu kusafiri na kufanya kazi katika kanda.

"Ninapokabidhi uenyekiti kwa kiongozi atakayenifuata, ninafanya hivyo nikiwa na imani kubwa katika mustakabali wa jumuiya yetu, Mustatakabali wa Afrika mashariki ni mzuri, kwa umoja wa dhamira, kuheshimiana na kujitolea kwa dhati tutaendelea kujenga kanda yenye ustawi, amani na mshikamano" amesema.

Katika mkutano huo maalumu uliohudhuriwa na Wakuu wa Nchi na 

Wajumbe Mashuhuri, amechaguliwa Katibu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Stephen Pateick Mbundi(Tanzania) akichukua nafasi ya aliyemaliza muda wake Bi.Veronica Nduva (Kenya).

Katika namna hiyohiyo Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika mashariki Rais Yoweri Museveni amepokea kijiti kutoka kwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Rais William Ruto amesisitiza  mshikamano wa wananchama na kusukuma mbele ajenda za ushirikiano wa kiuchumi biashara na kikanda.

"Kama hatutaunda soko kubwa na la kuaminika kwa wajasiliamali wetu, biashara haziwezi kukua, kuzalisha bidhaa nyingi, kuunda ajira zaidi au kulipa kodi, kutumia vizuri ardhi, anga na bahari" amesema Rais Mseveni.

Mwisho.

  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post