Na Lydia Lugakila-Misalaba MediaMBEYA Machi 07, 2026- Taasisi ya Tulia Trust, chini ya Mkurugenzi wake ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, imekabidhi nyumba mpya ya kuishi kwa familia ya Mzee Tuli Mwalwala Mwantindili.Nyumba hiyo imejengwa kupitia mpango wa “Tulia Trust Mtaani Kwetu”, na imekabidhiwa leo kwa familia hiyo inayoshi Mtaa wa Itongo, Kata ya Mwakibete, Jimbo la Uyole jijini Mbeya. Nyumba hiyo ni ya 23 kujengwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kusaidia wananchi wenye uhitaji, ambapo nyumba nne (4) kati ya hizo zimejengwa nje ya Jiji la Mbeya.Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba hiyo, Dkt. Tulia Ackson aliwahimiza wananchi wa kata hiyo kuendelea kuwa na utamaduni wa kusaidiana na kushirikiana kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili baadhi ya wananchi katika maeneo wanayoishi.“Sisi kama jamii tuendelee kushirikiana na kusaidiana katika changamoto mbalimbali tulizonazo, hata kwa kidogo tulichonacho,” amesema Dkt. Tulia.Mpango wa Tulia Trust Mtaani Kwetu unaendelea kusaidia jamii kwa kutoa makazi bora kwa watu wenye uhitaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo mbalimbali.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment