" NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA MKOANI MBEYA, APONGEZA UJENZI WA VITUO VYA POLISI MBEYA

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA MKOANI MBEYA, APONGEZA UJENZI WA VITUO VYA POLISI MBEYA

Na Lydia Lugakila-Misalaba Media Mbeya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mahmoud, leo Machi 07, 2026 amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mbeya, ambapo amekutana na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Mheshimiwa Jaffar Haniu, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyounda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kupokea taarifa za utendaji kazi.Katika ziara hiyo, Mhe. Mahmoud alikagua Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kipolisi Mbalizi kilichopo eneo la Utengule Usongwe, na kupongeza usimamizi pamoja na juhudi za wananchi waliojitolea kushiriki katika ujenzi wa kituo hicho.Aidha, amepokea taarifa ya miradi ya ujenzi wa vituo vya polisi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga. Taarifa hiyo imeeleza miradi iliyokamilika ambayo ni pamoja na vituo vya Polisi Makongolosi, Kambikatoto, Sangambi na Igoma.Vilevile, Mhe. Mahmoud alisomewa taarifa ya miradi ya ujenzi wa vituo vya polisi inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za ndani za halmashauri, ikiwemo mradi wa Kituo cha Polisi Igawa na Utengule Usangu katika Wilaya ya Mbarali, pamoja na mradi wa Kituo cha Polisi Ikuti katika Wilaya ya Rungwe.Mhe. Mahmoud amepongeza juhudi za wananchi na wadau mbalimbali wanaojitolea katika miradi ya ujenzi wa vituo vya polisi, na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo. Amesema lengo la Serikali ni kuboresha na kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi, ikiwa ni pamoja na kufikia azma ya kuwa na Kituo cha Polisi katika kila kata, ili kuzuia na kutokomeza uhalifu.


  

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post