DESK & Chair Foundation ya Jijini Mwanza imewanunulia nguo watoto yatima 100 ili waweze kutumia katika sherehe za Idi Elftri wakiwa na furaha kama wengine kwenye jamii.
Mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation, Sibstain Meghjee alisema Leo Jijini Mwanza kuwa wameona katika kipindi hiki cha sherehe baada ya Mfungo wa sikukuu ya Ramadhan wawanunulie watoto yatima nguo, viatu, madaftari, kalamu na kuwaandalia fursa ya kula nao chakula cha futari.
Alisema watoto wanaowahudumia wamefiwa baadhi na wazazi wao wote ama mmoja wakiwa ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 na wamewakutanisha katika msikiti wa Shede uliopo kata ya Mkuyuni kwa ajili ya kuwapatia mahitaji waliyo wachukulia.
Meghjee aliendelea kuiomba jamii kuwa na tabia ya kusaidia watoto waishio katika mazingira magumu kwani wanahitaji Kama Wengine ya kila siku ya kuwawezesha kukidhi mambo mhimu ya kimaisha.
Alisema kundi la watoto hao wamekatiwa bima za afya kwa ajili kuzitumia kukidhi mahitaji yao ya kimatibabu kila siku vilevile wanawasaidia kuweza kumudu masomo yao kwa kuwapatia fedha na kuwanunulia sare za shule.
"Tunawasaida baadhi na kuwalipia kodi za nyumba za kuishi hivyo tunafarijika kuwa watashiriki kwa furaha kwenye sikukuu ya Ramadhan" alisema Meghjee.
Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya Desk and Chair, Hisbat Mustaka alisema wamewagawia watoto wa kiume suruali za jeans, shati na viatu huku wasichana wamepewa gauni na viatu.
Aliongeza kusema kuwa vilevile tukio hilo la kugawa vifaa kwa watoto kwa sherehe limeenda sambamba na kufanya matibabu ya wagonjwa wa macho wapatao 28 kwenye hospitali ya Agarwals ambapo zaidi ya milioni 7 zimetumika.



Post a Comment