" KATIBU UVCCM PANGANI AANZA ZIARA YA “OPERESHENI SAMIA” KUWAFIKIA WANANCHI

KATIBU UVCCM PANGANI AANZA ZIARA YA “OPERESHENI SAMIA” KUWAFIKIA WANANCHI


Na: Mwandishi Wetu, Pangani

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Pangani, Mhe. Nasri Mkalipa, ameanza ziara maalum ya kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi, ziara hiyo ikiwa imepewa jina la “Operesheni Samia.”

Ziara hiyo ilianza Machi 24, 2026, katika Kata za Mkalamo na Mkwaja, ambapo Mkalipa aliweza kuonana na makundi mbalimbali ya kijamii, utaratibu uliopo wa CCM wa kuwafikia wananchi kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zao kwa wakati.


Akiwa ziarani, Mkalipa aliwahimiza vijana kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri. “Vijana wenzangu, tujiunge katika vikundi ili tuweze kunufaika na mikopo. Rais wetu na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatoa fedha nyingi za mikopo; ni jukumu letu kuchangamkia fursa hizi,” alisema.


Aidha, Mkalipa aliwataka vijana kujiandaa kwa ujio wa mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la Aweso Vijana Cup, mashindano yanayolenga kukuza vipaji na mshikamano miongoni mwa vijana.

Katika hatua nyingine, Mkalipa alisisitiza kuwa CCM ni chama imara, kinachoaminika na wananchi wake kutokana na sera zake zinazogusa maisha ya kila mmoja. Ziara ya siku tisa ya “Operesheni Samia” itafika katika Kata zote 14 za wilaya ya Pangani.




Post a Comment

Previous Post Next Post