Na Lydia Lugakila-Misalaba media Mbeya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameungana na waumini wa dini ya Kiislamu katika Baraza la Sikukuu ya Eid lililofanyika jijini Mbeya.Baraza hilo lilifanyika katika ukumbi wa City Garden, likiwakutanisha pamoja viongozi wa serikali, viongozi wa dini na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo kusherehekea sikukuu ya Eid kwa pamoja.Akizungumza katika hafla hiyo, Mhandisi Mahundi aliwapongeza waumini wa Kiislamu kwa kufanikiwa kukamilisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuwataka kuendelea kudumisha amani, mshikamano na upendo ndani ya jamii.Amesema kuwa Serikali inaendelea kuthamini mchango mkubwa wa viongozi wa dini katika kukuza maadili mema na kuimarisha umoja wa kitaifa. Aidha, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wa dini walieleza kufurahishwa na ushiriki wa viongozi wa serikali katika matukio ya kijamii na kidini, wakisema hatua hiyo inaongeza ukaribu na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya serikali na wananchi.Baraza hilo lilihitimishwa kwa dua maalum za kuliombea taifa amani, umoja na maendeleo.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254










Post a Comment