" MAONO YA RAIS SAMIA YAFUNGUA MILANGO YA NEEMA: MIRADI 876 YA CHINA YAZALISHA AJIRA MAELFU KWA WATANZANIA

MAONO YA RAIS SAMIA YAFUNGUA MILANGO YA NEEMA: MIRADI 876 YA CHINA YAZALISHA AJIRA MAELFU KWA WATANZANIA


Maono ya kimkakati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameendelea kuivusha Tanzania kiuchumi, ambapo ushirikiano wa kidiplomasia na nchi ya China sasa umezalisha miradi ya uwekezaji 876 yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 8,860 nchini. 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Machi 22, 2026, amebainisha kuwa uwekezaji huo ni matokeo ya mazingira rafiki yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita, jambo ambalo limesaidia kuzalisha ajira 146,250 kwa Watanzania.

 Mafanikio haya ni sehemu ya utekelezaji wa maono ya Rais Samia yaliyoanza tangu ziara yake ya kihistoria nchini China mwaka 2022, iliyoweka misingi imara ya ushirikiano wa kibiashara unaozidi kuimarika kila uchao.

Wakati huo huo, takwimu za biashara zinaonyesha kuwa mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenda China yameongezeka kwa asilimia 12.5, huku kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kikifikia dola bilioni 2. Hatua hii inathibitisha kuwa maono ya Rais Samia yanailenga Tanzania kuwa mshindani mkuu katika soko la kimataifa, huku yakichochea ukuaji wa viwanda vya ndani.

Waziri Kapinga amesisitiza kuwa mwenendo huu chanya ni sehemu ya maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050, inayolenga kukuza uchumi wa Tanzania kufikia thamani ya dola trilioni moja, huku sekta binafsi ikitarajiwa kubeba mzigo mkubwa wa asilimia 70 ya uwekezaji wote nchini.

Katika kuelekea malengo hayo, ziara ya Waziri Kapinga imewakutanisha jumla ya kampuni 150 za nchini China ambazo tayari zimewekeza au zina nia ya kuwekeza nchini Tanzania, ambapo Machi 21 kampuni 100 zilikutana  na nyingine 50 zimekutana Machi 22 kujadiliana fursa mpya. 

Wakati uwekezaji huu wa nje ukishika kasi, serikali imewekeza pia zaidi ya shilingi trilioni moja ndani ya nchi kuboresha usafiri wa majini katika maziwa na Bahari ya Hindi ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za wawekezaji na wakulima. Miradi hii inajumuisha ujenzi wa meli nne za mizigo katika Bandari ya Karema kwa ushirikiano na kampuni ya Gold Voyage Logistics ya China, hatua itakayofungua masoko ya nchi jirani kama DRC na Zambia.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post