Na Paul Kayanda, KahamaTarehe 15 Machi 2026, Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Benjamin Lukubha Ngayiwa ameandaa futari maalum kwa waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi mbalimbali wa eneo hilo. Tukio hilo limefanyika katika hali ya upendo, mshikamano na kuheshimiana kati ya jamii na Mbunge mwenyewe Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh wa Wilaya ya Kahama Omary Damka alimpongeza Mbunge huyo kwa moyo wake wa kujali na kuwakumbuka waumini wa Kiislamu katika kipindi hiki kitukufu cha Mwezi wa Ramadhani. Alisema kitendo hicho kinaonesha mshikamano na upendo kwa wananchi bila kujali tofauti za dini au makundi ya kisiasa.Sheikh Damka pia aliwakumbusha waumini wa Kiislamu umuhimu wa kudumisha mahusiano mema katika jamii, kuendelea kuheshimiana, kusaidiana na kuishi kwa amani na upendo wakati wote.Wananchi waliohudhuria futari hiyo walionesha furaha na shukrani zao kwa Mbunge Benjamin Ngayiwa kwa kuandaa tukio hilo, wakisema limeimarisha umoja na mshikamano katika jamii ya Kahama na kumsii nafanye hivyo na wakati mwingine.Kwa ujumla, futari hiyo imekuwa ishara nzuri ya mshikamano wa kijamii na kuthibitisha kuwa ushirikiano na upendo vina nafasi kubwa katika kujenga jamii yenye amani na maendeleo.Hata hivyo Mbunge Ngayiwa amesema amefanya hivyo Kama Mbunge Wa Jimbo Hilo lengo ni kukutanisha makundi yote ya walio Madini na wasio na dini Kwa kuwa ni wananchi wake anaowatumikia ambapo wamepata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo Kama familia Moja.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment