" MBUNGE PATALI ASISITIZA USIMAMIZI MAKINI WA MIRADI YA BARABARA MBEYA

MBUNGE PATALI ASISITIZA USIMAMIZI MAKINI WA MIRADI YA BARABARA MBEYA

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media

Mbeya

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, mhe. Patali Shida Patali, amesisitiza umuhimu wa usimamizi makini wa miradi ya barabara ili kuhakikisha thamani ya fedha inapatikana na miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango vinavyokidhi mahitaji ya Wananchi.

Mhe. Patali ametoa msisitizo huo aliposhiriki kikao cha bodi ya Barabara kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kilicholenga kujadili maendeleo ya miundombinu ya barabara mkoani Mbeya.

Katika kikao hicho, wajumbe wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo mipango ya matengenezo, ukarabati na uboreshaji wa barabara katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Mbeya, kwa lengo la kuboresha mtandao wa usafiri.

Lengo kuu la majadiliano hayo lilikuwa kuimarisha miundombinu ya Barabara ili kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi pamoja na kuchochea maendeleo ya Mkoa.

Ushiriki wa mbunge huyo katika kikao hicho unaendelea kuonesha dhamira yake ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Mbeya Vijijini na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla.

 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post