" MBUNGE WA JIMBO LA MPANDA MJINI MH.HAIDARY HEMED SUMRY NA MJUMBE WA BARAZA LA WAZAZI TAIFA KUTOKA MKOA WA KATAVI AKUTANA NA BARAZA LA WAZAZI CCM MPANDA MJINI.

MBUNGE WA JIMBO LA MPANDA MJINI MH.HAIDARY HEMED SUMRY NA MJUMBE WA BARAZA LA WAZAZI TAIFA KUTOKA MKOA WA KATAVI AKUTANA NA BARAZA LA WAZAZI CCM MPANDA MJINI.

Mbunge WA JIMBO LA MPANDA MJINI Ndg. HAIDARY HEMED SUMRY akizungumza na Baraza la wazazi CCM Jimbo la mpanda mjini katika WILAYA YA MPANDA 02/03/2026.

MBUNGE wa Jimbo la Mpanda Mjini Haidary Sumry amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Manispaa ya Mpanda ni kielelezo cha dhati kwa serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dkt Samia Suluhu kwa kusogeza huduma karibu na wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Haidary Sumry amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Manispaa ya Mpanda ni kielelezo cha dhati kwa serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dkt Samia Suluhu kwa kusogeza huduma karibu na wananchi.

Akizungumnza na Wajumbe wa Baraza la wazazi wa CCM Wilaya ya Mpanda kwenye ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kwenye uchaguzi wa Oktoba Mwaka Jana.


Sumry amesema kuwa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Barabara,Elimu,Kilimo,Maji pamoja na sekta nyingine umeongeza tija kwa wananchi kwa kusogezwa huduma hizo kwenye maeneo yao.

Katika Sekta ya Barabara kwenye manispaa ya Mpanda amesema ujenzi wa barabara wa kilomita 8.49 kupitia mradi wa TACTIC  ambao utekelezaji wake umeanza kwa wakandarasi kuanza kujenga kambi kwaajili ya kuanza kutekeleza mradi huo utakaonufaisha baadhi ya kata utakuwa ni mfano wa kuigwa kwa kujengwa Barabara za kisasa zitakazo pendezesha manispaa ya Mpanda kwa kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 21.

‘’Kwenye hili namshukuru sana Rais wetu Dkt Samia suluhu Hassan mwanzoni kulikuwa na kusuasua kwa utiaji sahihi wa mkabata huu lakini kabla ya uchaguzi wakati wa Kampeni Rais wetu alipokuja kuomba kura hapa Mpanda nilisimama na kumuomba kutia msukumo wa utiaji saini wa mkataba huo baada ya muda mkataba huo ulisainiwa na wakandarasi tayari wapo eneo la mradi na kazi inaendelea’’ anasema Haidary


Katika hatua nyiningine amewaomba wakazi wa Manispaa ya Mpanda kuupokea mradi huo wa barabara kwenye maeneo yao pindi utakapo anza kwakuwa ni bahati pekee waliyoipata kutoka kwa Rais Dkt Samia suluhu Hassan.

‘’Tukiwaona watalamu wetu wa ujenzi wa barabara wanaweka alama kwenye maeneo yetu huko tusishangae tufahamu ndio utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizo umeanza’’amesema Haidary

Katika sekta ya Maji amesema mradi wa maji wa Miji 28 unaojengwa katika Kata ya Shanwe ambao unagharimu zaidi ya Bilioni 22 unakwenda kuondoa adha ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda pindi utakapo kamilika.


Mradi huo ambao umefikia asilimia 55 unakwenda kuwa muarobaini kwa huduma ya maji kwa wanachi wa Manispaa ya Mpanda kwa kuondokana na tatizo la huduma ya Maji.

Katika Sekta ya Kilimo Haidary amesema serikali kuwekeza Bilioni 33 kwenye mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika Kata ya Mwamkulu ni mkombozi mkubwa kwa wakulima wa kata hiyo na Manispa kwa ujumla.

‘’Tulifanya ziara kwenye eneo hilo la mradi wa umwagiliaji kiukweli mradi huo unaendelea vizuri umefikia asilimia 70 na kukamilika kwa mradi huu wa umwagiliaji ni mapinduzi makubwa ya sekta ya kilimo kwa wanachi wetu wa Manispa ya Mpanda’’ amebainisha Haidary

Kuhusu Sekta ya Elimu amesema serikali imetekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa shule za sekondari kwa kuleta fedha nyingi kwa nyakati tofauti tofauti kwenye Manispaa ya Mpanda kubwa zaidi ni kujengwa kwa sekondari ya Wavuala ya Kanda Katavi katika Kata ya Kasokola yenye zaidi ya Bilioni 4 ambayo itaongeza chachu ya maendeleo ya sekta ya Elimu.

Amewaomba Wanachi wa Manispaa ya Mpanda kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano kwa kuwa maendeleo yanakwenda pamoja na umoja amani na mshikamano.

Kikao hicho cha Wajumbe wa Baraza la Wzazi Wilaya Mpanda ni mwendelezo wa utaratibu wa kukutana na makundi mbalimbali ya wanachi unaoendelea kufanywa na mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Haidary Sumry ambapo tayari ameshakutana na Wajumbe wa UWT Wilaya ya Mpanda na leo anatarajia kukutana na wajumbe wa umoja wa Vijana UVCCM Wilaya ya Mpanda.Katibu WA CCM WILAYA YA MPANDA Ndg. MUSA RAMADHAN MWEVI akiwasalimia wajumbe Wa Baraza la wazazi CCM Jimbo la mpanda mjini.Mwenyekiti Wa JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MPANDA Ndg. Pius Buzumalle akiwasalimia na kuwakaribisha  wajumbe Wa Baraza hilo la wazazi CCM Jimbo la mpanda mjini 02/03/2026.

Wenyeviti wa JUMUIYA ya WAZAZI CCM kata, makatibu wazazi CCM kata na makatibu ELIMU, MALEZI NA MAZINGIRA CCM kata wote 02/03/2026 wameshirikiki kikamilifu Baraza la wazazi CCM Jimbo la mpanda mjini katika WILAYA YA MPANDA.





 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post