Wanafunzi wa Shule ya Msingi
Nhelegani iliyopo mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuepuka kuvuka barabara wanapoona magari ya dharura yakipita.
Akitoa elimu hiyo, askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amesema kuwa magari ya dharura ni yale yanayotoa huduma za kuokoa maisha na kulinda usalama wa umma. Magari hayo ni pamoja na ya kubebea wagonjwa, zimamoto na polisi.
Amefafanua kuwa magari ya dharura hupaswa kuwa na ving’ora au taa za bluu na nyekundu zinazomulika ili yapatiwe kipaumbele barabarani.
Aidha, Sajenti Ndimila
amewasisitiza wanafunzi hao kuongeza umakini wanapotaka kuvuka barabara, pindi wanapokuwa kwenye kivuko cha watembea kwa miguu, wanapaswa kutoa kipaumbele kwa magari ya dharura kupita kwanza.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment