*Baraka Kifumbe* *Mwanza* Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Kwimba imenufaika na mgao wa vifaa na mashine za Kisasa unaolenga kuongeza tija kwenye ufundishaji na kukuza elimu ya ufundi stadi Nchini.Akiongea kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika leo Jijini Mwanza , Mkuu wa Chuo - VETA Kwimba Bwana Elias Msigwa amesema kuwa, Chuo cha Kwimba ni wanufaika wa mgao wa vifaa na mashine za kisasa zitakazotumika kwenye kufundishia wanafunzi ili kuleta tija kwenye kutoa elimu ya ufundi chuoni hapo.Bwana Msigwa amesema anaishukuru Serikali pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Antony Mzee Kasore kwenye kuhakikisha vifaa vya kisasa vinapatikana ili kuboresha ufundishaji na kuleta tija kwenye elimu ya ufundi.Msingwa ameongeza kuwa, VETA Kwimba inejipanga kutekeleza vyema majukumu yake kwenye kupanua fursa za chuo cha Kwimba ikiwemo kuwawezesha watu wenye mahitaji maalumu kupata fursa za masomo kupitia kuondoa malipo ya ada kwa watu wenye wenye ulemavu.Pia Msigwa amewaomba waandishi wa habari kuendelea kuitangaza VETA ili jamii ifahamu huduma zinazotolewa na chuoo hicho.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment