Kahama
Mtoto Nicholaus Meshack (9), mkazi wa Mtaa wa Shunu, Manispaa ya Kahama, amerejea nyumbani akiwa anaweza kutembea mwenyewe baada ya kupatiwa matibabu maalum katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) iliyopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha anapatiwa matibabu na Serikali kugharamia gharama zote.
Nicholaus amepata changamoto ya kiafya takribani miaka miwili iliyopita baada ya kuvunjika mguu alipokuwa akicheza na wenzake shuleni, Licha ya kupatiwa matibabu ya awali, hali yake ilizidi kuwa mbaya na kufikia hatua ya kushindwa kutembea kabisa na Mama yake amelazimika kuomba msaada kupitia vyombo vya habari mwezi Januari mwaka huu.
Baada ya taarifa hiyo kufikishwa kwa mamlaka husika, mtoto huyo alipokelewa MOI Januari 5 na kuanza matibabu mara moja, Akiwa hospitalini hapo, alifanyiwa upasuaji mara mbili, akaendelea na tiba ya mazoezi (physiotherapy) pamoja na kupatiwa dawa maalum.
Muuguzi kutoka MOI, Ritha Makundi, amesema wakati wanampokea Nicholaus hakuwa akitembea wala kujitegemea, lakini baada ya matibabu na uangalizi wa karibu hali yake imeimarika kwa kiasi kikubwa.
“Alipofika Hospitali kwetu alikuwa hawezi kutembea kabisa, lakini baada ya kupatiwa matibabu sasa anaweza kutembea mwenyewe bila kutumia vifaa saidizi,” amesema.
Afisa Ustawi wa Jamii wa MOI, Theresia Tarimo, ameeleza kuwa mtoto huyo amepewa dawa za kuendelea kutumia nyumbani na ameshauriwa kurejea hospitalini baada ya miezi mitatu kwa uchunguzi wa ufuatiliaji.
Akizungumza kwa niaba ya familia, mama wa mtoto huyo, Lucia Kawawa, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugusa na kufuatilia kwa karibu suala la mwanaye hadi kuhakikisha anapatiwa matibabu stahiki.
Kwa upande wake, Nicholaus ameishukuru Serikali kupitia Rais Samia kwa msaada alioupata, akionyesha furaha yake kwa kurejea nyumbani akiwa katika hali nzuri na matumaini ya kurejea shuleni.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment