Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza mkakati wa kufungamanisha usafiri wa majini na nchi kavu kupitia ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR na bandari kavu ili kuongeza ufanisi wa usafirishaji.
Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, akizungumza na waandishi wa habari mjini Mwanza ameeleza kuwa ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 39.21 na mradi huo umekamilika na kuanza kufanya kazi.
Pia amesema Serikali tayari imetoa maeneo katika bandari hiyo kwa ajili ya nchi za Rwanda, DRC, Burundi, Zambia, Uganda, Malawi, Sudan Kusini na Zimbabwe ili kurahisisha huduma zao za shehena.
Aidha, TRC inaendelea na upembuzi yakinifu ili kuunganisha reli ya SGR na bandari hiyo ya Kwala.
Katika hatua nyingine, serikali imeanza maandalizi ya kuanzisha Bandari Kavu mkoani Morogoro itakayohudumia shehena ya mizigo inayosafirishwa kwa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam. Mradi huu unalenga kuongeza matumizi ya reli na kupunguza gharama za usafirishaji huku ukilinda barabara zetu.
Sambamba na hilo, uboreshaji wa bandari za maziwa unaendelea ambapo mradi wa Bandari ya Mbamba Bay Ziwa Nyasa unagharimu shilingi bilioni 75.85, huku shilingi bilioni 26.42 zikitengwa kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Vilevile, uboreshaji wa Bandari ya Kigoma unafanyika kwa ushirikiano na Japan kupitia Shirika la JICA.
Muunganiko huu wa reli na bandari kavu ni nguzo muhimu katika kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uchukuzi Afrika Mashariki.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment