Serikali imezindua kampeni maalum ya chanjo ya Polio
mkoani Shinyanga kufuatia kuwepo kwa hatari ya maambukizi ya ugonjwa huo, baada
ya kubainika kwa vimelea vyake katika maji taka jijini Mwanza.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, amesema hatua hiyo imelenga kuzuia kusambaa
kwa ugonjwa wa Polio ambao hauna tiba, bali unazuilika kwa njia ya chanjo.
Amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni salama kwa watoto wote
walio chini ya umri wa miaka 10, huku akionya kuwa mtoto atakayekosa chanjo
atakuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga,
CP. Salum Hamduni, amewataka wazazi na walezi kujitokeza kwa wingi kuhakikisha
watoto wote wanapatiwa chanjo hiyo muhimu ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa
Polio unaoweza kusababisha ulemavu wa kudumu au hata kifo.
Akizungumza Machi 23, 2026 katika kikao kazi cha
hamasa ya kampeni hiyo, Hamduni amesema zoezi la utoaji chanjo litafanyika
kuanzia Machi 24 hadi 27, 2026, likilenga kuwafikia watoto 781,166 wenye umri
chini ya miaka 10 mkoani humo.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameipongeza
Serikali kwa jitihada zake za kulinda afya ya watoto, wakieleza kuwa uwekezaji
katika afya ya mtoto ni msingi muhimu wa kulinda kizazi cha sasa na cha
baadaye, pamoja na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





































Post a Comment