" TANZANIA IPO KIKAZI ZAIDI, BUNGE , WATU BINAFSI NA SERIKALI WASHIKAMANA MAJI

TANZANIA IPO KIKAZI ZAIDI, BUNGE , WATU BINAFSI NA SERIKALI WASHIKAMANA MAJI


Ile ndoto ya "kumtua mama ndoo kichwani" sasa inakwenda kuwa kweli kwa kasi ya ajabu baada ya mhimili wa Bunge na matajiri wa sekta binafsi (TPSF) kuamua kuungana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kusafisha njia ya maji nchini kote. Huu siyo mchongo wa maneno tena, bali ni mwendo wa vitendo ambapo mabilioni ya fedha na teknolojia ya kisasa vimeelekezwa vijijini na mijini ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji salama bombani.

Akizungumza kwa msisitizo kwenye kilele cha Wiki ya Maji mjini Morogoro, Spika wa Bunge, Mussa Zungu, amewasha taa ya kijani kwa serikali akisema Bunge halitarudisha nyuma hitaji lolote la kifedha linalolenga kuleta maji kwa wananchi.

 Zungu amewahakikishia vijana na wakazi wa vijijini kuwa Rais Samia amekuja na suluhisho la kudumu kwa kufufua miradi mikubwa kama wa Kidunda, uliokuwa umelala tangu mwaka 2001, ili lita milioni 600 za maji zinazopotea baharini sasa zije kuwahudumia wananchi.

"Bunge litaunga mkono juhudi zote na mahitaji ya serikali hii kuhakikisha wananchi wanapata maji salama," alisema Spika Zungu, akionyesha kuwa mhimili huo umeamua "kuepika" na serikali ili matokeo yaonekane haraka mitaani.

Kwa upande wa vijana wanaotafuta fursa, Sekta Binafsi (TPSF) imekuja na habari njema ya ajira na uwekezaji. Mjumbe wa Bodi ya TPSF, Ngwisa Mpembe, amebainisha kuwa katika miaka mitano iliyopita, takribani Sh trilioni 1.2 zimewekezwa na sekta binafsi kwenye viwanda vya vifaa vya maji.

Mpembe akifafanua zaidi alisema, sekta binafsi kupitia TPSF inafanya mambo matano makubwa ya kuleta mageuzi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya maji na kuanzisha viwanda vya ndani vya kuzalisha vifaa kama mabomba na pampu. 

Kwa TPSF kuanzisha viwanda zaidi vitakavyozalisha pampu na vifaa vya ujenzi, pamoja na kuwezesha miradi ya maji kuendelea kutekelezwa pia jambo hilo litazalisha ajira nyingi kwa vijana na wanawake, huku wakileta teknolojia za kijanja kama "mita janja" na uvunaji wa maji ya mvua ili kupunguza gharama za maji.

Mpembe amesisitiza kuwa maboresho ya sera na mifumo ya kodi yaliyofanywa na serikali yamewapa wawekezaji ujasiri wa kuingia mtaani na kuweka mitaji yao kwenye miradi ya maji vijijini. Hii ina maana kuwa huduma za maji sasa hazitategemea bajeti ya serikali pekee, bali nguvu ya wafanyabiashara wakubwa pia imeelekezwa huko ili kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu na ya kisasa.

Mshikamano huu wa Bunge na Sekta Binafsi unatoa ujumbe mmoja thabiti kwa watu wa vijijini na vijana wa mjini: Serikali yenu haiko peke yake, na injini ya maendeleo imewashwa kikamilifu. 

Kupitia ushirikiano huu, Tanzania inakwenda kuondokana na kero ya maji, ikitengeneza mazingira ya afya bora na fursa za kujiingizia kipato kwa kila mwananchi, bila kuacha mtu nyuma.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post