Lydia Lugakila-Misalaba Media, MbeyaWananchi wa Kata ya Ilemi Jijini Mbeya wametakiwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za ulinzi wa maeneo yao ili kusaidia kuzuia vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza katika mitaa wanayoishi.Mkaguzi wa Polisi wa Kata ya Ilemi, Elibariki Mambuye, ametoa wito huo Machi 07, 2026 wakati Kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo ilipofanya ziara katika mitaa sita ya kata hiyo kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi pamoja na kuboresha utoaji wa huduma.Katika ziara hiyo, Mambuye amesisitiza kuwa ushiriki wa wananchi katika masuala ya ulinzi na usalama ni muhimu kwa kuwawezesha vyombo vya dola kudhibiti uhalifu mapema.Aidha, amewahimiza vijana wanaojihusisha na biashara ya bodaboda kuwa mabalozi wazuri wa usalama katika maeneo yao kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pindi wanapobaini watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo uporaji wa mikoba na simu za mkononi.Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Ilemi, Baraka Zambi, amewataka wazazi na walezi kuongeza umakini katika ulinzi na usalama wa watoto hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepuka matukio ya watoto kusombwa na maji au kutumbukia kwenye visima na mabwawa.Zambi ameongeza kuwa yeye pamoja na kamati yake wataendelea kushirikiana na wananchi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo ubovu wa barabara, ukosefu wa kivuko cha watembea kwa miguu pamoja na ombi la kuongezwa Shule ya Msingi katika eneo la Ilindi Lyoto kutokana na ongezeko la idadi ya wananchi linalosababisha shule iliyopo sasa kuzidiwa.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment