" WANAWAKE WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI NA UONGOZI KATAVI

WANAWAKE WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI NA UONGOZI KATAVI

 

Wanawake mkoani Katavi wamehimizwa kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii huku wakitambua nafasi na mchango wao muhimu katika familia na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Hoza Mrindoko, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake, ambapo alisisitiza umuhimu wa kulinda haki za wanawake, kuwawezesha kiuchumi pamoja na kuwapa nafasi zaidi za kushiriki katika uongozi na maamuzi ya maendeleo.

Mrindoko amesema mwanamke ana nafasi kubwa katika kujenga familia imara na jamii yenye maadili, hivyo ni muhimu kuhakikisha wanawake wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na wanapewa fursa sawa katika elimu, ajira na shughuli za kiuchumi.

Amesema serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wanawake kwa kutoa mikopo ya kuwawezesha kiuchumi pamoja na kuimarisha mifumo ya bima ya afya ili kuhakikisha wanawake na familia zao wanapata huduma bora za afya.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano katika jamii huku akiwataka wazazi kuendelea kutoa malezi bora kwa watoto na kuhakikisha wanapelekwa shule ili kupata elimu itakayowasaidia kujenga maisha bora ya baadaye.

Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, Jimotoli Jilala, amesema jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika kuhamasisha jamii kuthamini nafasi ya mwanamke pamoja na kuhimiza wazazi kuwalea watoto katika maadili mema na kuhakikisha wanapata elimu.

Amesema jamii inapaswa kuendelea kuimarisha mshikamano na ushirikiano katika malezi ya watoto na kuwapa wanawake nafasi ya kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kuleta ustawi wa familia na taifa kwa ujumla.



 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



 

Post a Comment

Previous Post Next Post