" Azam FC Yaendeleza Ubabe Dhidi ya Simba

Azam FC Yaendeleza Ubabe Dhidi ya Simba




NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Wakati Wakristo wakisherehekea Sikukuu ya Pasaka inayoendana na kumbukumbu ya tukio la kufufuka kwa Bwana Yesu, Jiji la Dar es Salaam sherehe hizo zitanogeshwa na mechi kali ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Azam dhidi ya Simba uliopigwa leo, Aprili 5, 2026, katika dimba la Azam Complex, huku timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana (0-0).

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa huku kila upande ukijitahidi kutafuta ushindi, lakini safu za ulinzi za timu zote zilikuwa imara na kuzuia hatari zote zilizojitokeza. Simba walionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo hasa kipindi cha pili, lakini walishindwa kutumia nafasi walizopata.

Kwa upande wa Azam FC, walicheza kwa nidhamu kubwa wakilenga mashambulizi ya kushtukiza, lakini nao pia hawakufanikiwa kupenya ukuta wa ulinzi wa wapinzani wao.

Wenyeji wa mchezo huo Azam wanaonolewa na kocha Mkongomani, Florent Ibenge, ambapo wametoshana nguvu dhidi ya vijana wa kocha Steve Barker, Simba.

Ulikuwa sio mechi ya kawaida kwani imezikutanisha timu mbili zinazofukuzana kwa ukaribu katika mbio za ubingwa, huku kila mmoja akihitaji pointi tatu ili kuwakaribia vinara, Yanga.

Kufuatia matokeo hayo Simba kwa sasa inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 35 baada ya mechi 16, huku ikiwa na faida ya mechi moja mkononi dhidi ya mpinzani wake wa jadi, Yanga, mwenye alama 41. kwa upande wa Azam, ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 baada ya mechi 17.

Post a Comment

Previous Post Next Post