
Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) Bavoo Junus,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mawakili wa Serikali Tanzania, Ado Novemba,akizungumza katika mkutano wa mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha mawakili wa serikali uliofanyika leo Aprili 29,2026 jijini Dodoma.
...
Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt. Juma Homera, amewataka mawakili wa Serikali nchini kuongeza umakini na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuilinda Serikali dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na uzembe au usimamizi usio madhubuti wa mashauri ya kisheria.
Akizungumza katika Kikao kazi cha mawakili wa serikali, Dkt.Homera amesema kuwa kazi ya uwakili wa Serikali ni mhimili muhimu katika kulinda rasilimali za taifa na kuhakikisha haki inatendeka kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na sheria.
“Ni wajibu wenu kuhakikisha kila shauri linasimamiwa kwa umakini wa hali ya juu. Uzembe mdogo unaweza kusababisha hasara kubwa kwa Serikali na wananchi kwa ujumla,” amesema Dkt.Homera.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amekipongeza Chama cha Mawakili wa Serikali (TPBA) kwa kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama wake, akibainisha kuwa hali hiyo ni msingi muhimu wa kuimarisha taaluma na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Amesisitiza haja ya kuendelea kuijenga na kuimarisha taasisi hiyo kuanzia ngazi ya chini hadi taifa kwa kuweka mifumo madhubuti ya kiutendaji itakayowezesha chama hicho kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.
Dkt.Homera amebainisha kuwa TPBA inapaswa kuwa na muundo thabiti unaojumuisha wataalamu wenye weledi pamoja na sekretarieti imara, ili iweze kutoa huduma bora kwa wanachama wake na kuisaidia Serikali katika masuala ya kisheria.
Aidha, amependekeza kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa maendeleo wa chama hicho, utakaolenga kuboresha ustawi wa wanachama wake na kuhakikisha uendelevu wa shughuli zake kwa muda mrefu.
Waziri Homera amesisitiza kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuthamini mchango wa mawakili wa Serikali katika kulinda utawala wa sheria na kusimamia ipasavyo rasilimali za umma.
Ameongeza kuwa mchango huo ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi kwa Serikali na kuhakikisha kuwa haki na usawa vinazingatiwa katika utoaji wa huduma za kisheria nchini.
Post a Comment