📌 *REA Yapongezwa uhamasishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia* .
📌 *Umeme sasa ni kitongoji kwa kitongoji*
📍 *Iwambi, Mbeya* .
Tamasha la Kilimo lililokuwa likifanyika mkoani Mbeya limehitimishwa rasmi leo Jumatano, tarehe 29 Aprili 2026, kwa mafanikio makubwa huku likiwa limekusanya wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, nishati na maendeleo kutoka ndani na nje ya mkoa huo. Tamasha hilo limekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kuonesha teknolojia mpya na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu njia bora za kuboresha maisha yao kupitia kilimo na matumizi sahihi ya nishati.
Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga tamasha hilo,mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu ameipongeza REA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya matumizi ya nishati safi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ina mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi na kulinda mazingira. Alieleza kuwa matumizi ya nishati safi kama majiko ya umeme, majiko ya gesi na majiko banifu yanasaidia kupunguza athari za moshi unaotokana na kuni na mkaa, ambao umeendelea kuwa chanzo cha magonjwa ya mfumo wa upumuaji hususan kwa wanawake na watoto.
“Ni muhimu kwa wananchi kuendelea kukumbatia matumizi ya nishati safi ya kupikia. Hii siyo tu inalinda afya zetu, bali pia inachangia katika uhifadhi wa mazingira yetu kwa kupunguza ukataji wa miti ovyo,” alisema mgeni rasmi.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa REA kuendelea kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme vijijini ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi zaidi wanapata huduma hiyo muhimu ambayo ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Alibainisha kuwa upatikanaji wa umeme unarahisisha matumizi ya teknolojia mbalimbali za kisasa, ikiwemo majiko ya umeme, ambayo ni rafiki kwa mazingira na gharama nafuu kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine, mgeni rasmi alizishukuru taasisi zote za serikali na binafsi, pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika tamasha hilo kwa kujitokeza kwa wingi na kuonesha bidhaa na huduma zao. Alieleza kuwa ushiriki huo umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya tamasha hilo na kutoa fursa kwa wananchi kupata elimu na maarifa yatakayowasaidia kuboresha shughuli zao za kila siku.
Aliongeza kuwa maonesho kama hayo yanapaswa kuendelezwa na kupewa kipaumbele, kwani yana nafasi muhimu ya kuunganisha watu kutoka maeneo mbalimbali, kubadilishana mawazo na kuibua fursa mpya za maendeleo. “Tamasha hili limekuwa ni daraja la kuwaunganisha wadau na wananchi, na ninaamini elimu iliyotolewa hapa itakuwa chachu ya maendeleo endelevu kwa jamii,” alisisitiza.
Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa tamasha hilo walieleza kufurahishwa na namna walivyopata elimu kuhusu teknolojia mpya za kilimo na nishati safi, wakiahidi kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata. Walisema kuwa kupitia maonesho hayo, wamepata uelewa mpana zaidi kuhusu faida za kutumia majiko ya kisasa na umuhimu wa kuachana na matumizi ya nishati zisizo rafiki kwa mazingira.
Tamasha la Kilimo la mwaka huu limeacha alama kubwa kwa wakazi wa Mbeya na maeneo jirani, likiwa limefanikiwa si tu kuhamasisha maendeleo ya kilimo, bali pia kukuza uelewa wa matumizi ya nishati safi na uhifadhi wa mazingira. Wadau wengi wameeleza matumaini yao kuwa matukio kama haya yataendelea kufanyika mara kwa mara ili kuendeleza kasi ya maendeleo nchini.
*Mwisho.*
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment