Na Lydia Lugakila-Misalaba Media Mbeya Waumini walioguswa na moto wa Roho Mtakatifu wetakiwa kuishi maisha yenye heshima na kuonyesha tofauti katika mwenendo wao wa kila siku na kutokukubali moto wa Mungu uzimike katika maisha yao.Kauli hiyo imetolewa na mtumishi wa Mungu, Mchungaji Thobias Tambikeni wakati akiwahubili waumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) Forest ya kwanza Mkoani Mbeya katika ibada iliyofanyika Aprili 26, 2026 kanisani hapo.Mchungaji Tambikeni alisisitiza umuhimu wa kuweka uhusiano na Mungu mbele ya kila jambo, akieleza kuwa msingi wa imani ya kweli ni kupokea na kulitunza neno la Mungu .Alionya kwamba waumini wanaopuuzia maandiko matakatifu wanajiweka katika hatari ya kupotea kiroho, na kuwataka kuhakikisha wanatunza moto wa Mungu.Katika mahubiri yake, alifafanua kuwa wokovu wa kweli unahitaji nidhamu, utii na moyo wa kujitoa kikamilifu kwa Mungu. Mchungaji Tambikeni alieleza kwa masikitiko kuwa baadhi ya waumini wameacha misingi ya maombi na kufunga. Alisisitiza kuwa yeyote anayehitaji nguvu ya Mungu hana budi kuheshimu na kushika neno lake kwa bidii.Pia alikumbusha kuwa moto wa Mungu ni ishara ya uwepo Wake, na unapaswa kuwaka daima bila kuzimika. Akiiwahimiza waumini kulinda na kudumisha moto huo kwa gharama yoyote, hasa katika nyakati hizi ngumu zinazohitaji imani hai.Akizungumzia wajibu wa viongozi wa kiroho, alisema kuwa kazi ya mchungaji ni kuhakikisha madhabahu inaendelea kuwaka moto wa Mungu. Alionya kuwa wengi wanajikwaa kwa sababu ya kukosa moto huo, huku akisisitiza kuwa moto wa Mungu ni Roho Mtakatifu na bila Yeye ni vigumu kumfikia Mungu.Aidha, alihimiza uwekezaji wa kweli katika uhusiano na Mungu kupitia maombi, kujitoa na maisha ya unyenyekevu. Pia alikemea tabia ya kuishi kwa kanuni nyingi zisizo na msingi wa kiroho, hasa ndani ya familia, akisema hali hiyo huzuia nuru ya Mungu kufanya kazi. Mchungaji Tambikeni alisisitiza kuwa moto wa Mungu unapaswa kuanzia nyumbani, na kwamba Mungu huvutwa na viwango vya kiroho vya mtu. Alibainisha kuwa moto wa Mungu huzaa huduma, na huduma hujenga Ukristo wa kweli.Ameongeza kuwa yeyote anayetamani nguvu za Mungu lazima amtafute kwa bidii, kwa kuwa nguvu hiyo huambatana na moto wake popote aendapo.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment