" MWENYEKITI BARAZA LA WAZEE SHINYANGA ATOA WITO WA AMANI KATIKA KUIMARISHA MUUNGANO NA MAENDELEO YA TAIFA

MWENYEKITI BARAZA LA WAZEE SHINYANGA ATOA WITO WA AMANI KATIKA KUIMARISHA MUUNGANO NA MAENDELEO YA TAIFA

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano, ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, amesisitiza umuhimu wa amani kama msingi mkuu wa kudumisha Muungano na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Akitoa simulizi ya kihistoria, mzee huyo amesema wakati Muungano unapatikana alikuwa na umri wa takribani miaka 10, akieleza kuwa tangu wakati huo Tanzania imeendelea kujengwa katika misingi ya amani, mshikamano na umoja wa kitaifa.

Amebainisha kuwa amani iliyojengwa na waasisi wa Taifa, ikiwemo viongozi wa awali wa nchi, imekuwa nguzo muhimu inayolinda Muungano na kuwezesha maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Amesema kuwa bila amani, Muungano usingeweza kudumu kwa mafanikio yaliyopo sasa, akiwataka Watanzania wote kuendelea kuuenzi na kuulinda kwa nguvu zote kama urithi wa thamani kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha, amesisitiza kuwa wazee wana jukumu la pekee la kutoa busara na historia kwa vijana ili kuwajenga katika misingi ya uzalendo, umoja na utulivu, akibainisha kuwa jamii yenye amani hujenga taifa imara na lenye maendeleo endelevu.

Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kulinda amani na mshikamano wa kitaifa kama nguzo kuu ya kuendeleza mafanikio ya Muungano na ustawi wa nchi kwa ujumla.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post