NA: MWANDISHI WETU, MPWAPWA Wananchi 156,000 kutoka vijiji 23, shule 11 na vituo vya afya 10 vya wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji, ambao una mchango mkubwa katika kuwaondolea adha ya kufuata maji umbali mrefu.Hayo yameelezwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wilayani humo wakati wa uzinduzi wa mradi wa "Badilisha Maisha Mpwapwa," unaogharimu shilingi bilioni 30, ambao utawasaidia wananchi kuwaondolea changamoto ya maji katika maeneo yao."Mradi huu una mchango mkubwa katika kuhakikisha wananchi wa Mpwapwa na vijiji vyake wanapata maji safi, salama na yenye kutosheleza,"amesema Aweso.Katika hatua nyingine, Aweso amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030, vijiji 1,575 visivyo na huduma ya maji vinapata maji ili kila mwananchi afurahie maji kwa matumizi mbalimbali.Vilevile, Aweso amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa miundombinu ya maji huku vituo 255 vya kuchotea maji vikitarajiwa kujengwa.Kimsingi, mradi huo ni matokeo ya ushirikiano kati ya serikali na Shirika la Water For People Tanzania, ambapo kukamilika kwake ni kutachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Ikumbukwe kuwa dhamira ya serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuwezesha wananchi wote kupata huduma ya maji ikizingatia kuwa maji ni muhimu katika maisha ya binadamu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment