Vituo vya maendeleo ya mtoto na kijana katika Klasta ya Shinyanga vimezindua mtaala wa Mama wa Upendo pamoja na program ya Alpha, hatua inayolenga kuimarisha malezi ya kiroho kwa watoto na vijana na kuwasaidia kufuata misingi sahihi ya maisha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwezeshaji wa
Klasta ya Shinyanga na Kahama, Bwana Remi Dumbi, alisema miongozo hiyo imelenga
kuwawezesha wamama wa upendo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi katika
kuwalea na kuwaombea watoto pamoja na vijana.
Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuwaombea vijana katika
kila hatua ya maisha yao, akibainisha kuwa hata wanapofikisha umri wa miaka 20
na kuendelea bado wanahitaji maombi na uongozi wa kiroho.
“Lengo letu la kwanza ni kuhakikisha vijana wanamjua Yesu na kufuata njia
sahihi. Wamama wa upendo wamekuwa mstari wa mbele katika maombi na
tunawashukuru kwa hilo,” alisema.
Aliongeza kuwa mtaala wa Mama wa Upendo unahusisha
masuala ya utume wa mama, majukumu yao, namna ya kufundisha, vipindi pamoja na
mbinu za kushirikiana na watendakazi katika kuwalea vijana na kubaini maono
yao.
Kwa upande wa program ya Alpha, Dumbi alisema Klasta
hiyo imeingia makubaliano na shirika la Alpha tangu mwezi Machi kwa lengo la
kuwafikia vijana ambao mara nyingi hawapendi kuhudhuria ibada makanisani.
Alisema kupitia program hiyo, vijana hao wanatafutwa na kuandaliwa mazingira
rafiki ya kuwavuta na kuwasaidia kumjua Yesu.
Aidha, Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Steven
Chinyongolo, aliwataka vijana kutumia fursa hiyo kujijenga kiroho na kuwa na
hofu ya Mungu katika maisha yao, huku akiwahimiza wamama wa upendo kuendelea
kuwa nguzo muhimu katika malezi ya kizazi kijacho.
Naye Mchungaji Odras aliwataka washiriki wa tukio hilo
kumtumaini Mungu na kuomba uongozi wake katika utekelezaji wa mtaala huo,
akisisitiza kuwa malezi ya kiroho ni msingi muhimu wa maisha ya mwanadamu na
yanapaswa kupewa kipaumbele.
Wakati huo huo, Wamama wa Upendo wa huduma ya Esta
Encounter katika Klasta ya Shinyanga wameeleza mafanikio, changamoto na
matarajio yao katika kuimarisha huduma ya mtoto na kijana, wakisisitiza umuhimu
wa ushiriki wa wanawake wa Kikristo katika malezi na ulinzi wa watoto.
Huduma hiyo ilianzishwa mwaka 2008 na Mchungaji
Emmanuel Mbennal, aliyekuwa Mkurugenzi wa Nchi wa Compassion International
Tanzania, kwa lengo la kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika huduma
ya watoto na vijana kupitia maombi, malezi na ushauri wa kijamii.
Wamama hao wamesema wamefanikiwa kuunda uongozi,
kuendesha mikutano ya maombi ya mara kwa mara na kushiriki katika shughuli za
kuwalea na kuwaombea watoto na vijana, huku wakiimarisha mshikamano kwa
kusaidiana wakati wa changamoto.
Hata hivyo, wamebainisha changamoto zinazowakabili
kuwa ni pamoja na mwitikio mdogo wa baadhi ya wanachama, ukosefu wa fedha za
usafiri, ushirikiano hafifu kutoka baadhi ya watendakazi pamoja na uhaba wa
vitabu vya muongozo wa huduma.
Pamoja na changamoto hizo, wamama hao wameeleza kuwa
wanaendelea kushikamana na kuamini kuwa kupitia umoja na ushirikiano, huduma
hiyo itaendelea kukua na kuleta matokeo chanya kwa watoto na vijana katika
jamii.
Mchungaji Odras Gunda
Bwana REMI DUMBI Mwezeshaji wa klasta ya Shinyanga na Kahama
Askofu Steven Chinyongolo. Askofu wa anglican church of Tanzania 

Afisa ustawi wa jamii wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Lydia Kwesigabo akizungumza.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



























Post a Comment