" SIDO YACHOCHEA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI KAHAMA

SIDO YACHOCHEA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI KAHAMA

Na Paul Kayanda, KahamaSHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO) limewahamasisha wananchi na wadau wa maendeleo katika Wilaya ya Kahama kujitokeza kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya kutengeneza mkaa mbadala kutoka kwenye taka ambayo ni mapumba ya mpunga  hatua inayolenga kulinda mazingira na kukuza uchumi wa wananchi.Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Teknolojia na Viwanda wa SIDO, Mhandisi Kalumuna Benedicto, wakati wa mafunzo maalum yaliyofanyika katikà Manispaa ya  Kahama, ambapo alieleza kuwa teknolojia hiyo ni suluhisho la kudumu la kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa wa asili.Alisema SIDO kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO), chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan, wanatekeleza mradi wa kuzalisha mkaa mbadala kwa kutumia taka mbalimbali kwa gharama nafuu, huku wajasiriamali wakipatiwa mashine za kisasa za uzalishaji.“Teknolojia hii inatumia malighafi inayopatikana kirahisi kama taka za majumbani na mapumba ya mpunga, hivyo kutoa nishati safi ya kupikia, kuongeza kipato kwa wananchi na kulinda mazingira,” alisema Benedicto.Aliongeza kuwa Kahama ina fursa kubwa ya kufanikisha mradi huo kutokana na wingi wa taka zinazotokana na uzalishaji wa mpunga, hasa mapumba yanayotumika kama malighafi kuu ya mkaa huo mbadala.Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walieleza kufurahishwa na mradi huo, wakisema ni fursa muhimu ya kiuchumi na kimazingira. Bakari Kile alisema kuwa uwekezaji huo utasaidia kupunguza utegemezi wa kuni ambao bado unatumika kwa zaidi ya asilimia 90 ya wananchi.“Teknolojia hii ni jibu la changamoto za mabadiliko ya tabianchi na pia itasaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya taifa na dunia,” alisema.Washiriki walitoa wito kwa taasisi husika kuongeza elimu kwa wananchi, hasa maeneo ya vijijini, ili kuongeza uelewa na matumizi ya nishati hiyo mbadala. Pia waliwashauri wananchi kutembelea vituo vya mfano kama kampuni ya Dorfla ili kujifunza zaidi kuhusu matumizi ya mashine hizo.Akizungumza kwa niaba ya washiriki, Mathias Charles kutoka Kata ya Ngaya alisema bado kuna uelewa mdogo kuhusu matumizi ya mkaa mbadala kutokana na uhaba wa majiko maalum, na kusisitiza haja ya elimu zaidi.Kwa upande wake, Mzee Abdu Mhamed alisisitiza kuwa pamoja na uwekezaji katika uzalishaji, ni muhimu pia kuwekeza katika elimu ya matumizi sahihi ya nishati hiyo ili kuondoa kabisa utegemezi wa kuni na mkaa wa asili.Mratibu wa mradi kutoka UNIDO, Faustene Msangira, alisema mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Shinyanga (Kahama), Morogoro (Kilosa) na Mbeya tangu mwaka jana, ukiwa na lengo la kupunguza ukataji wa miti na uharibifu wa mazingira.Alibainisha kuwa mradi huo unatarajiwa kuwa chachu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, huku ukiwawezesha wananchi kiuchumi na kulinda rasilimali za asili kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post