" Sababu ya Bei ya Mafuta kushuka Katika Soko la Dunia

Sababu ya Bei ya Mafuta kushuka Katika Soko la Dunia

 

Bei ya Mafuta Zashuka Katika Soko la Dunia
Bei za mafuta zimeshuka kwa kasi katika Soko la Dunia huku hati fungani zikipanda na masoko ya hisa yakiongezeka baada ya makubaliano ya usitishaji vita kwa wiki mbili unaohusisha Iran kuchochea hali ya matumaini sokoni huku Wawekezaji wakifurahia uwezekano wa kuanza tena kwa usafirishaji wa mafuta na gesi kupitia Mlango wa Hormuz.

Rais wa Marekani, Donald Trump alisema mwishoni mwa Jumanne wiki hii kuwa amekubaliana kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa wiki mbili na kuongeza kuwa makubaliano ya amani ya muda mrefu yako katika hatua za maandalizi.

Iran ilisema itasitisha mashambulizi yake ikiwa mashambulizi dhidi yake pia yatasimama na kwamba usafiri salama kupitia Mlango wa Hormuz utawezekana kwa wiki mbili kwa kushirikiana na Jeshi la Iran.

Masoko ya dunia yamekuwa yakitetereka tangu Marekani na Israel zilipoishambulia Iran mwishoni mwa Februari hali iliyosababisha Tehran kufunga kwa kiasi kikubwa Mlango wa Hormuz ambayo ni njia muhimu inayotumika kusafirisha takribani asilimia 20 ya mafuta na gesi ya dunia.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post