" SIMBA YAICHAPA YANGA 1-0, YASEPA NA KOMBE LA MUUNGANO 2026

SIMBA YAICHAPA YANGA 1-0, YASEPA NA KOMBE LA MUUNGANO 2026

 Klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga SC katika fainali ya Kombe la Muungano, na kuondoka na kitita cha shilingi milioni 150.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika kwa sare ndani ya dakika 90 za kawaida, hali iliyolazimu kuongezwa kwa muda wa nyongeza wa dakika 30 ili kupata mshindi.

Bao pekee la ushindi lilipatikana katika dakika za nyongeza kupitia mshambuliaji wa Simba, Selemani Mwalimu, aliyefunga kwa mkwaju wa penalti na kuihakikishia timu yake ushindi muhimu.

Ushindi huo umeifanya Simba kutwaa ubingwa wa michuano hiyo huku Yanga wakilazimika kukubali kipigo katika pambano hilo kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post