Akizungumza kwenye maadhimisho ya maonesho ya kimataifa ya Afya na Usalama Mahali Pa kazi ambayo huandaliwa na (OSHA) yanayoendelea Mkoani Njombe , Mtendaji Mkuu wa (ATE) Bi. Suzanne Ndomba – Doran amesema ni muhimu kwa waajiri nchini kuzingatia na kutekeleza Sheria ya Usalama na Afya kazini kwa kuweka mifumo madhubuti ya OSHA inayolinda usalama wa kimwili na kisaikolojia kama sehemu ya usimamizi wa biashara.
“Mazingira bora ya kazi kisaikolojia ni njia bora ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na kujenga taasisi imara”, amesema Bi. Ndomba
Ameongeza kuwa usalama wa kisaikolojia muhimu ili kuondoa msongo wa mawazo , uchovu wa kupindukia pamoja na hofu ni hatari ambazo zinaweza kuzuilika endapo zitawekewa mipango madhubuti ili kuongeza ufanisi mahali pa kazi.
“Endapo kazi zitapangwa kwa ufanisi na majukumu kubainishwa wazi bila kuathiri utendaji na tija kazini,”
“Na Kujenga utamaduni wa “Kinga Kwanza” kwa kujumuisha hatari za kisaikolojia (mfano msongo wa mawazo na uchovu wa kupindukia) katika tathmini za hatari na upangaji wa kazi zinaweza kuleta matokeo Chanya kwa nchini kwa ujumla,” amefafanua.
Amesema maadhimisho ni siku muhimu kwamba mafanikio ya uchumi hayawezi kupimwa kwa tija pekee, bali pia kwa usalama, afya na utu wa wafanyakazi.
Bi Ndomba amesema kwa mujibu wa Taarifa ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) ya mwaka 2026, hatari za kisaikolojia kazini kama msongo wa mawazo kazini husababisha upotevu wa takribani asilimia 1.37 ya Pato la Taifa (GDP) duniani kila mwaka.
“Hii ni hasara kubwa inayoweza kuzuilika pale waajiri wanapowekeza katika Usalama na Afya Kazini,’ amesema Bi. Ndomba.
Ametoa wito kwa Serikali; kuimarisha uratibu kati ya OSHA na mamlaka nyingine ili kuongeza ufanisi na kupunguza mwingiliano wa majukumu.na kuweka mifumo ya utekelezaji iliyo rafiki kwa biashara bila kushusha viwango vya usalama na afya kazini.
Ameongeza kuwa ni muhimu pamoja na mambo mengine Kuwekeza katika elimu, uhamasishaji na uimarishaji wa uwezo, hususan kwa biashara ndogo na za kati, kwa kushirikiana na waajiri na wafanyakazi.
Bi Ndomba amewashukuru waajiri wote waliowezesha na kushiriki kikamilifu katika maonesho ya Usalama na Afya kazini.
“Ushiriki wenu unaonesha kwa vitendo dhamira ya kuwekeza kwenye teknolojia, bunifu na mbinu bora za kulinda usalama, afya na ustawi wa wafanyakazi,’ amesisitiza.
Maonesho ya Afya na Usalama mahali pa kazi ambayo hufanyika kila mwaka huandaliwa na Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) na kauli mbiu ya mwaka huu ni Mazingira Bora ya Kazi Kisaikolojia ni Njia ya Kuimarisha Ustawi wa Wafanyakazi na Kujenga Taasisi Imara.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254















Post a Comment