" WAKAZI WA MBEYA WAJIPANGA KWA PRE-BETIKA MBEYA TULIA MARATHON 2026

WAKAZI WA MBEYA WAJIPANGA KWA PRE-BETIKA MBEYA TULIA MARATHON 2026


Na Lyidia Lugakila - Mbeya

Wakazi wa Jiji la Mbeya wameanza kujipanga kikamilifu kushiriki mbio za Pre-Betika Mbeya Tulia Marathon 2026, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mashindano makubwa ya riadha yanayotarajiwa kufanyika tarehe 15 hadi 16 Mei mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine, mkoani Mbeya.

Shughuli hiyo ya maandalizi imevutia makundi mbalimbali ya wananchi, wakiwemo wanariadha wa kitaalamu na wale wa kawaida, ambao wameonyesha hamasa kubwa ya kushiriki katika tukio hilo lenye lengo la kuhamasisha afya bora pamoja na mshikamano wa kijamii.

Waandaaji wa mashindano hayo wameeleza kuwa Pre-Marathon inalenga kuwajengea washiriki uwezo wa kujiandaa kimwili na kiakili kabla ya siku rasmi ya mashindano, huku wakisisitiza umuhimu wa mazoezi ya mara kwa mara ili kuhakikisha ushiriki wenye mafanikio.

Aidha, imeelezwa kuwa Betika Mbeya Tulia Marathon 2026 inalenga pia kuchangisha fedha zitakazotumika kusaidia jamii, hususan katika sekta za afya, elimu na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Baadhi ya wakazi wa Mbeya wamepongeza juhudi hizo, wakisema kuwa mashindano hayo sio tu yanakuza vipaji vya michezo, bali pia yanatoa fursa ya kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuvuta washiriki kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, na hivyo kuongeza chachu ya maendeleo ya michezo pamoja na utalii katika mkoa wa Mbeya.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post