" WATANZANIA TUDUMISHE AMANI, TUEPUKE KUGAWANYIKA KWA MASLAHI YA WACHACHE

WATANZANIA TUDUMISHE AMANI, TUEPUKE KUGAWANYIKA KWA MASLAHI YA WACHACHE


Na Mwandishi Maalum

Nawapongeza kwa dhati Watanzania kwa kuendelea kudumisha umoja wa kitaifa, amani na mshikamano katika kipindi hiki tunapoendelea na mchakato wa maridhiano ya Kitaifa yanayolenga kuwaleta Watanzania wote pamoja  bila kujadili dini, itikadi, ukanda au misingi mingine yoyote inayoweza kuwagawa Watanzania.

Nyakati hizi zenye vishawishi vingi kutoka nje ya nchi zinapaswa kuepukwa na Watanzania wote kwa maslahi ya Mama Tanzania, ukweli ni kwamba hatuna taifa jingine la kukimbilia ikiwa tutavuruga amani iliyopo, inayotufanya tutembee kifua mbele na kuwa kivutio Duniani kote kwa kuwa tumekuwa kisiwa cha amani kwa miongo mingi sasa na tumeendelea hivyo hata sasa.

Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa aliwahi kusisitiza kuwa “Urithi mkubwa tulioachiwa na waasisi wetu ni amani. Jukumu letu la kila kizazi kuilinda na kuikabidhi kwa kizazi kijacho ikiwa salama”, msisitizo huu unatupa wajibu kuwa amani ni jukumu letu sote bila kujali itikadi zetu.

Hayati Benjamin Mkapa katika moja ya hotuba zake wakati akiaga Ikulu Jijini Dar es Salaam alisema, ”Tumejenga Tanzania kwa misingi ya amani, umoja na mshikamano. Msingi huu tusiubomoe, tuulinde kama tulindavyo mboni za macho yetu”, huu ulikuwa ujumbe wake wa mwisho kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tukiwa tumegawanyika tu dhaifu; tukiwa wamoja, Afrika inaweza kuwa na nguvu mojawapo kubwa duniani”, Baba wa Taifa la Ghana Kwame Nkurumah akisisitiza kuhusu umoja na mshikamano jinsi unavyoweza kuchangia katika kuleta maendeleo kwa Waafrika, Tanzania ni sehemu ya Bara la Afrika ambayo imetoa mchango mkubwa katika bara hili na dunia kwa ujumla katika kuimarisha amani.

Nkurumah anaendea kusisitiza kuwa, “bila  umoja hakuna nguvu, bila nguvu hakuna maendeleo, bila maendeleo hakuna heshima,” muhimu hapa ni kutambua kuwa umoja ni msingin wa kujenga maridhiano na Taifa letu hasa nyakati hizi tunazopitia ambazo miluzi kutoka nje imekuwa ikitaka kuleta mgawanyiko kati yetu kupitia kwa wanaharakati wa ndani na wale wanaoishi nje ya Tanzania.

Tanzania ikiwa taifa lenye rasilimali nyingi ikiwemo madini adimu, gesi asilia, misitu, wanyama, chuma na vingine vingi imekuwa moja ya eneo ambalo mataifa mengi ya nje yanalitamani kwa sababu ya utajiri huu. 

Kuwepo kwa rasilimali hizi kumeipa Tanzania marafiki na hata washirika wengi wa maendeleo na pia wapo wachache wanaotamani kutumia changamoto zetu kama mtaji wa kujipatia rasilimali zetu kwa njia zisizokubalika ikiwemo kuvuruga amani iliyopo.

Bara la Afrika linajivunia utajiri mkubwa na rasilimali nyingi, Tanzania ikiwemo, “Afrika itaandika historia yake yenyewe, na itakuwa, kaskazini na kusini mwa sahara, historia ya utukufu na heshima”, Patrice Lumumba.

Mara kadhaa tumewasikia viongozi wetu wa Dini akiwemo Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Dkt. Fredrick Shoo wakisisitiza kuwa Watanzania tuna jukumu la kujenga umoja, maridhiano na mshikamano kwa kuwa njia tayari tunayo yakulifikia jambo hilo.

Tanzania ni nchi inayotajwa kuwa imejenga uwezo wa kutatua changamoto zake yenyewe pale zinapojitokeza na imekuwa nyakati zote mfano katika Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla kwa kushiriki katika utatuzi wa migogoro ikiwemo ya nchi za Maziwa Makuu, Kusini mwa Afrika, Afrika kwa ujumla na duniani kwa njia mbalimbali ikiwemo kuchangia vikosi vya walinda amani, upatanishi na hata ukombozi wa kisiasa.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post