
Na Farida Mangube, Morogoro
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya mauaji yaliyotokea katika wilaya za Malinyi, Kilombero na Kilosa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi wa polisi ACP Andrew Gabriel Kantimbo amesema tukio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Nyameni, kata ya Ulaya wilayani Kilosa, ambapo mwanamke aitwaye Janeth Ernest Mazengo (52) alifariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa na mumewe, Amos Zakaria Kisomeko (64).
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alimshambulia marehemu kwa muda mrefu na kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake.
Katika tukio jingine lililotokea wilayani Kilombero ambapo Ramadhani Sadick Joseph (35) anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua Messe Germanus Ngayungwa (23) mkazi wa Ifakara, marehemu alidaiwa kupigwa na kitu kizito hadi kupoteza maisha, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa upelelezi wa matukio hayo unaendelea, na watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kufuata taratibu za kisheria pale wanapokumbana na migogoro, ili kuepuka matukio ya ukatili yanayoweza kusababisha vifo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment