
Watanzania wameaswa kulinda na kuenzi amani ya nchi kwa gharama zote, kwani ndiyo msingi mkuu unaowezesha uwepo wa haki na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Shehe wa Mkoa wa Mwanza na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani humo, Hassan Kabeke, amesisitiza kuwa uwepo wa utulivu unatoa fursa kwa kila mwananchi kutekeleza majukumu yake, ikiwemo viongozi wa dini kupata nafasi ya kusali, kuabudu, na kusifu kwa uhuru bila hofu yoyote.
Shehe Kabeke amebainisha kuwa amani na haki ni vitu vinavyoendana na haviwezi kutenganishwa, akieleza kuwa upatikanaji wa haki unategemea kuwepo kwa amani kwa kiasi kikubwa.
Amesema kuwa hata kama serikali itatekeleza wajibu wake wa kujenga miundombinu kama barabara, hospitali, na shule, huduma hizo hazitaweza kutumika endapo amani itatoweka, kwani wagonjwa hawatatibiwa na wanafunzi hawatasoma katika mazingira ya machafuko.
Kuhusu watu wanaobeza amani iliyopo, kiongozi huyo ameshauri kuwa wasichukiwe bali waendelee kuelimishwa kwa mifano halisi, akibainisha kuwa kama kusingekuwa na amani, wasingepata hata nafasi hiyo ya kukejeli utulivu uliopo.
Amewatahadharisha Watanzania kujiepusha na watu wenye nia ovu wanaochochea hamasa za kuvuruga nchi kwa kisingizio cha kutafuta haki, akisisitiza kuwa watu wa aina hiyo ni hatari na hawapaswi kupewa nafasi katika jamii kwa ustawi wa taifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment