Na Milu Malimi, Misalaba Media
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Shinyanga wameeleza namna vitendo vya rushwa vinavyoendelea kuathiri maendeleo ya jamii na kusababisha changamoto katika utoaji wa huduma za kijamii, hususan sekta ya afya.
Wakizungumza na Misalaba Media Mei 8, 2026, wananchi
hao wamesema vitendo vya utoaji na upokeaji wa rushwa vimekuwa vikijitokeza
katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma, ambapo baadhi ya watumishi huwapa
upendeleo wananchi wanaotoa rushwa na kuwaacha wengine kukosa haki zao za
msingi.
Miongoni mwa wananchi hao ni William Muhangwa, ambaye
amesema rushwa imeendelea kuwa changamoto katika maeneo ya huduma za kijamii
kama hospitali, shule na baadhi ya taasisi za umma, hali inayochangia wananchi
wengi kushindwa kupata huduma kwa usawa.
Ameeleza kuwa baadhi ya sababu zinazochochea vitendo
vya rushwa ni tamaa ya kujipatia fedha kwa njia zisizo halali, mishahara midogo
kwa baadhi ya watumishi pamoja na ukosefu wa uwajibikaji katika taasisi za
umma.
Aidha, wananchi hao wamewataka wananchi pamoja na
watumishi wa umma kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa ili kujenga jamii
yenye haki, usawa na maendeleo, wakisema rushwa imekuwa chanzo cha kudorora kwa
huduma za kijamii na kukosekana kwa haki kwa baadhi ya wananchi.
Pia wameeleza kuwa elimu kuhusu madhara ya rushwa
inapaswa kutolewa mara kwa mara kwa wananchi ili kuongeza uelewa wa jamii
kuhusu athari zake, huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali
na wananchi katika kuhakikisha vitendo vya rushwa vinakomeshwa.
Hata hivyo, wamezitaka taasisi zinazohusika na
mapambano dhidi ya rushwa kuongeza juhudi za kuchukua hatua kwa wanaojihusisha
na vitendo hivyo ili kulinda haki za wananchi na kuimarisha utoaji wa huduma za
kijamii nchini.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment