" AMANI NDIO MSINGI WA UBUNIFU WA VIJANA KATIKA KUFIKIA DIRA YA UCHUMI SHINDANI WA VIWANDA NA BIASHARA IFIKAPO 2050

AMANI NDIO MSINGI WA UBUNIFU WA VIJANA KATIKA KUFIKIA DIRA YA UCHUMI SHINDANI WA VIWANDA NA BIASHARA IFIKAPO 2050




Ukuaji wa biashara, ujasiriamali, na mnyororo wa thamani wa viwanda nchini unategemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa mazingira tulivu yanayomwezesha kijana kufikiri kwa uhuru na kuonesha ubunifu wake kikamilifu. 

Akizungumza katika kilele cha Jukwaa la Wiki ya Ukuaji katika Kazi na Bunifu za Biashara kwa Vijana lililoandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amebainisha kuwa serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ili vijana washiriki katika kujenga uchumi shindani kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Hata hivyo, ili juhudi hizi za kuweka mkazo katika uwekezaji wa rasilimali watu, elimu, teknolojia, na ujasiriamali zizae matunda, utulivu na usalama wa nchi ndio nguzo kuu inayoruhusu mifumo hiyo kufanya kazi bila mtikisiko.

Vijana lazima wazekee na kuzingatia kuwa hakuna kiwanda kinachoweza kuzalisha, wala taasisi ya kifedha inayoweza kukopesha, na hakuna jukwaa la kibiashara linaloweza kukutanisha wabunifu iwapo amani itatoweka.

Taifa lenye vijana wenye uwezo wa kujitegemea kiuchumi ndilo msingi wa maendeleo endelevu, lakini utegemezi huo unajengwa pale tu ambapo amani inalindwa ili kutoa fursa ya mawazo mapya kufanyiwa kazi kwa vitendo. 

Kaulimbiu ya jukwaa hilo inayohimiza ubunifu na ujuzi kwa vijana kama msingi wa ukuaji wa biashara na viwanda nchini, imebeba ujumbe mzito unaotaka nguvu kazi hii kubwa na hazina ya taifa iongozwe kwa nidhamu ya kazi, maarifa yanayotekelezeka, na uwezo wa kutatua changamoto za jamii. 

Katika ulimwengu wa sasa ambapo haitatosha kuwa na cheti pekee darasani, kijana anahitaji utulivu wa akili ili aweze kufikiri kwa ubunifu, kuwasiliana vizuri, na kushirikiana na wengine. Utulivu huo wa kijamii unapatikana pale tu ambapo vijana wanakuwa walinzi wa kwanza wa amani, wakitambua kuwa vurugu na machafuko huharibu miundombinu ya kiteknolojia na kufukuza wawekezaji wanaohitajika kukuza mawazo yao ya kibiashara.

Upande wake Mkuu wa CBE, Profesa Edda Lwoga, ameeleza kuwa jukwaa hilo ni daraja muhimu linalounganisha elimu ya darasani na mahitaji halisi ya soko la ajira kwa kuwapa wanafunzi nafasi ya kusikiliza wataalamu kutoka sekta za benki, atamizi za biashara, teknolojia, na uwezeshaji wa kiuchumi. 

Mijadala na mafunzo haya ya kimkakati yanayolenga kuwandaa vijana kwa ajili ya maisha ya kazi na ujasiriamali yanawezekana tu kwa sababu nchi ipo katika hali ya utulivu wa kisiasa na kijamii. 

Ni jukumu la vijana sasa kuchangamkia fursa hizi zinazoratibiwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuhakikisha wanalinda misingi ya umoja wa kitaifa, kwani ubunifu wowote wa kibiashara au kiteknolojia hauwezi kushamiri katika mazingira ya hofu na sintofahamu. Kujenga uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu ulio mseto na himilivu kunahitaji rasilimali watu yenye amani ya moyo na utulivu wa mazingira ili kuleta mapinduzi ya kweli ya viwanda.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post