Dereva bodaboda aliyefahamika kwa jina la Ally Kambi (24), mkazi wa Kingolwira Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kukodi huduma yake ya usafiri, kisha kuporwa pikipiki yake.
Tukio hilo linasadikika lilitokea katika eneo la Mkambarani Wilaya ya Morogoro, ambapo mwili wa marehemu ulipatikana porini ukiwa na majeraha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Andrew Kantimbo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na mauaji hayo.
Akizungumzia tukio hilo na Moja ya chomba Cha Habari baba mkubwa wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Shukuru Msonga amesema Ally aliondoka Mei 11, 2026 majira ya usiku baada ya kukodiwa na mtu asiyejulikana, lakini hakurejea nyumbani.
Msonga amesema baada ya kijana huyo kutorejea kwa siku nzima, familia ilitoa taarifa kwa Serikali ya mtaa na kituo cha polisi, ambapo juhudi za kumtafuta zilianza mara moja.
“Tulihangaika kumtafuta maeneo mbalimbali, tulifika hata hospitali na kutoa taarifa kwenye vijiwe vya bodaboda. Hatimaye jana asubuhi tukapata taarifa kuwa kuna mwili umeonekana porini,” amesema Msonga.
Amesema yeye pamoja na ndugu wengine walipofika eneo la tukio waliutambua mwili huo kuwa ni wa Ally Kambi. Mwili huo ulikuwa na majeraha, huku pembeni kukiwa na fimbo kubwa (gongo) pamoja na fulana iliyokuwa imelowa damu.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo huku juhudi za kuwatafuta watuhumiwa zikiendelea.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment