" DIWANI ATOA MILIONI 3.3 KUFANIKISHA SHEREHE NA UJENZI WA MIUNDOMBINU KANISANI

DIWANI ATOA MILIONI 3.3 KUFANIKISHA SHEREHE NA UJENZI WA MIUNDOMBINU KANISANI


Na Paul Kayanda, KahamaDIWANI wa Kata ya Majengo katika Manispaa ya Kahama Mkoa wa Shinyanga, Zacharia Soko, ameonyesha moyo wa kujitoa na kuunga mkono shughuli za maendeleo ya Kanisa Katoliki kwa kutoa mchango wa  shilingi milioni 1.3 kwa ajili ya kufanikisha sherehe ya Siku ya Somo  Parokia ya Roho Mtakatifu Majengo, Jimbo Katoliki la Kahama, zinazotarajiwa kufanyika Mei 24, 2026.Mbali na mchango huo, Diwani Soko amesema kuwa kama kiongozi wa wananchi wa Kata ya Majengo, ameona umuhimu wa kushiriki maendeleo ya kiroho na kijamii ya waumini kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu mbalimbali ndani ya eneo la kanisa hilo.Akizungumza wakati wa harambee fupi iliyofanyika katika Parokia ya Roho Mtakatifu Majengo, Diwani Soko alisema kuwa ushirikiano kati ya viongozi na taasisi za dini ni msingi muhimu wa kuimarisha mshikamano wa jamii pamoja na maendeleo endelevu.“Kanisa lina nafasi kubwa katika kulea maadili mema kwa jamii yetu. Kama viongozi tunapaswa kushirikiana na taasisi za dini kuhakikisha shughuli zake zinaendelea vizuri na mazingira bora yanajengwa kwa manufaa ya waumini na wananchi kwa ujumla,” alisema Soko.Katika misa hiyo takatifu iliyowakutanisha waumini mbalimbali pamoja na viongozi wa dini na jamii, waumini walimpongeza Diwani huyo kwa moyo wake wa kujitoa na kuhamasisha maendeleo ya kanisa pamoja na jamii inayomzunguka.Sherehe ya Siku ya Somo Parokia  ya roho mtakatifu Majengo inayotarajiwa kufanyika Mei 24 mwaka huu inatarajiwa kukutanisha waumini kutoka maeneo mbalimbali ya Jimbo Katoliki la Kahama mgeni rasmi akitarajiwa kuwa askofu mkuu Wa Jimbo katoliki la Kahama Mhashamu baba Christopher Ndizeye  kwa lengo la kuimarisha imani, mshikamano na kuchangia maendeleo ya kanisa.Aidha, viongozi wa Parokia ya Roho Mtakatifu Majengo wamewataka wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kuchangia shughuli hiyo muhimu ili kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa mafanikio makubwa.Kwa upande wake Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu Majengo Padri Nobert Masuma ametoa shukrani za dhati kwa Diwani wa Kata ya Majengo, Zachari Soko, kwa moyo wake wa upendo na mchango mkubwa alioutoa kufanikisha maadhimisho ya Sikukuu ya Pentekoste yanayoadhimishwa katika Parokia ya Roho Mtakatifu iliyopo Kata ya Majengo siku ya mei 24,2026 huku akimtakia kheri katikà utendaji  uliotukuka Kwa wananchi WA Majengo.Akizungumza kwa niaba ya waumini wote wa parokia hiyo, padri Masuma amesema kuwa ushirikiano na majitoleo ya diwani huyo yameonyesha mfano wa uzalendo, mshikamano na kujali maendeleo ya kiroho na kijamii ya wananchi wa Majengo.“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Zachari Soko kwa moyo wake wa kujitoa na kuendelea kuwa karibu na Kanisa pamoja na waumini wake. Mungu ambariki kwa wema wake na azidi kumpa afya, hekima na mafanikio katika kuwatumikia wananchi,” alisema Paroko Masuma.Aidha, waumini wa Parokia ya Roho Mtakatifu Majengo wameeleza furaha yao kwa ushirikiano huo ambao umechangia kufanikisha maandalizi ya siku hiyo muhimu ya Pentekoste, wakisema kuwa matendo ya upendo na mshikamano huimarisha umoja katika jamii.Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwa ibada, nyimbo za sifa na shughuli mbalimbali za kiroho zitakazowakutanisha waumini pamoja na wageni kutoka maeneo mbalimbali.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post