Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuzuia ajali zisizo za lazima wawapo barabarani Akitoa elimu hiyo katika kituo Cha Polisi Wilaya ya Shinyanga Mkuu wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga Mrakibu msaidizi wa Polisi Zainabu Mangara amewataka madereva wa pikipiki kufuata Sheria za usalama barabarani pasipo shuruti ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya vyombo vyao moto, kuacha kubeba abiria zaidi ya mmoja kwenye pikipiki, kukata bima ya chombo Cha moto pamoja na kuheshimu watumiaji wengine wa barabara.Aidha Mangara amewaasa kuwa mabalozi wa usalama barabarani Kwa kukemeana wao Kwa wao kuacha vitendo visivyofaa kama kuharibu bomba la mfumo wa utoaji Moshi kitu kinachopelekea utoaji wa sauti za milipuko kwenye pikipiki.Kwa upande wao Maafisa usafirishaji hao wamelishukuru Jeshi la Polisi Kwa kuwapatia elimu hiyo na kukiri kuwa mabalozi wazuri wa kufuata Sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kupelekea vifo, majeruhi pamoja na uharibifu wa vyombo vya moto.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment