Na Edwin Soko, Mwanza
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Royal iliyopo jijini Mwanza inatarajiwa kufunguliwa rasmi leo Mei 10, 2026, hatua inayotarajiwa kuongeza upatikanaji wa huduma bora na za kisasa za afya kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa na maeneo ya jirani.
Ufunguzi huo unatarajiwa kufanyika leo huku mamia ya wananchi, viongozi wa dini, wadau wa sekta ya afya pamoja na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki tukio hilo muhimu katika sekta ya afya.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rev. Dr. Barnabas W. Mtokambali.
Ujio wa Hospitali hiyo ya Rufaa unaelezwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji huduma za kibingwa na za kisasa karibu zaidi na maeneo yao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Royal, Daktari Lusako Mwaikasu amesema maandalizi yote ya uzinduzi huo yamekamilika na wageni mbalimbali wamewasili tayari jijini Mwanza kushiriki hafla hiyo.
“Tunawakaribisha wananchi wote kushiriki siku hii muhimu ambapo rasmi tunaanza kutoa huduma kwa kiwango cha juu zaidi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla,” amesema Dkt. Mwaikasu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Daktari Glory Simon amesema hospitali hiyo imejipanga kutoa huduma bora, za kisasa na zenye viwango vinavyokidhi mahitaji ya wananchi.
Amesema uwepo wa Hospitali ya Rufaa ya Royal utasaidia kupunguza changamoto ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kibingwa.
Naye Bwana Richard Nickson kutoka Ghana ambaye yupo jijini Mwanza kwa ajili ya kushiriki uzinduzi huo, amesema wananchi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa wamepokea kwa furaha taarifa za kufunguliwa kwa hospitali hiyo kutokana na matarajio makubwa waliyonayo katika kuboresha huduma za afya.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Royal ipo Mtaa wa Ghana, jijini Mwanza.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment