" HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA YANG’ARA KITAIFA KWA KUSHIKA NAFASI YA PILI UTOAJI HUDUMA ZA AFYA

HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA YANG’ARA KITAIFA KWA KUSHIKA NAFASI YA PILI UTOAJI HUDUMA ZA AFYA

Na Mwandishi wetu Misalaba Media, Mbeya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya District, ndugu Tamim Kambona, amewataka wahudumu wa afya katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma ili hatimaye hospitali hiyo iwe ya kwanza kitaifa.Ameyasema hayo Mei 6, 2026 ofisini kwake wakati akikabidhiwa cheti cha pongezi kwa niaba ya hospitali hiyo, kufuatia ushindi wa kushika nafasi ya pili kitaifa katika utoaji wa huduma za afya, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya yaliyofanyika mkoani Pwani katika Halmashauri ya Kibiti.“Mwaka jana tulikuwa nafasi ya tatu, na mwaka huu tumeweza kupanda hadi nafasi ya pili. Hii inaonesha maendeleo mazuri, hivyo naomba muongeze kasi ya kuhudumia wananchi ili mwaka ujao tufikie nafasi ya kwanza kitaifa,” alisema Kambona.Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya, Dkt. John Gungumka, amesema wataendelea kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi ili kufikia malengo ya kuboresha huduma za afya wilayani humo.Dkt. Gungumka pia amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na viongozi wengine kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa kwa wahudumu wa afya, akisema msaada huo umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yaliyopatikana.Aidha, ameomba ushirikiano huo uendelee kuimarishwa ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa Chunya na Watanzania kwa ujumla wanaofika kupata huduma katika hospitali hiyo.Hospitali ya Wilaya ya Chunya imeibuka mshindi wa pili kitaifa kati ya hospitali za wilaya 167 zilizoshindanishwa, katika mashindano yaliyofanyika tarehe 29 Aprili 2026 katika Halmashauri ya Kibiti, mkoani Pwani.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post