
Moja ya hotuba ya kihistoria ya kuwatia moyo wananchi wa nchi hizi mbili katika safari ya kuelekea kwenye ushirikiano wa kweli kibiashara unaoashiria kuleta mafanikio ilitolewa na Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Azizi mbele ya Ma Rais wa nchi hizi, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dk.William Ruto.
Alisema wananchi wa wakenya na wa Tanzania wanapaswa kushirikiana na hakuna ambaye yupo juu ya mwenzake katika nyanja za biashara, mitaji na uchumi.
“Ni muhimu Wakenya kukubali kwamba Watanzania wamekua na tupo kimo kimoja hivyo tunapaswa kuchukua hatua na historia mpya katika muktadha wa kujenga mfungamano wa kweli wa kiuchumi na kubadilisha mustakabali wa nchini hizi mbili”, alisisitiza.
Rostam alisema muktadha huu mpya wa dunia, Tanzania na Kenya zina nafasi ya kipekee ya kimkakati, alisisitiza na kuongeza kuwa Wakenya waache kufurahia, kusherekea au kushabikia watanzania wanapopata majanga au taharuki mbalimbali na Watanzania wasiwaone Wakenya ni tishio kwenye biashara na ajira.
Alisema tunapakana na masoko mengi ya kikanda, tuna bandari muhimu katika Bahari ya Hindi, na tupo kwenye njia kuu za biashara za dunia. Kwa lugha rahisi, sisi ndiyo lango la biashara la Bara letu la Afrika.
Aliongeza kwamba ni nafasi ya kipekee kwa watanzania na wakenya kufanya kazi kwa kushirikiana na si kwa kutengana kwa sababu nchini hizi zinahitajiana.
Hotuba ya kusisitiza ushirikiano baina ya mataifa ya Tanzania sio mara ya kwanza kutolewa na mfanyabiashara huyu,hivi karibuni akiongea na waandishi wa habari jijini Nairobi alisema Tanzania na Kenya sio maadui na washindani bali zinapaswa kushirikiana na kusaidiana.
Aliongeza kwamba hakuna kaka mkubwa katika ushirikiano huo wa kibiashara na mitaji kati kenya na Tanzania bali wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kukuza mitaji , kuongeza ufanisi wa biashara , mitaji na uwekezaji mkubwa kwenye miradi yenye maslahi mapana kwa nchini hizo mbili.
Alisisitiza kwenye mkutano huo kwamba hakuna mkubwa dhidi ya mwenzake , watanzania na wakenya wote wapo sawa (we are equals).
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment