" JAJI MWAMBEGELE AWAPA NENO MAKARANI WA UCHAGUZI ISIMANI

JAJI MWAMBEGELE AWAPA NENO MAKARANI WA UCHAGUZI ISIMANI

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa  Mhe.Jacobs Mwambegele akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya siku moja kwa Makarani  waogozaji Wapiga Kura katika Jimbo la Isimani yaliyofanyika katika Shule Sekondari Ufundi Ifunda mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi huo utakaofanyika Jumatatu ya Juni 1, 2026.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa  Mhe.Jacobs Mwambegele amewataka watendaji wa uchaguzi ambao ni Makarani waongozaji Wapiga kura kufanya kazi yao kwa kufuata Sheria, Kanuni na utaratibu wakati wa uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Isimani Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara.

Jaji Mwambegele ameyasema hayo wakati akitembelea mafunzo ya siku moja kwa Makarani hao waogozaji katika Jimbo la Isimani yaliyofanyika katika Shule Sekondari Ufundi Ifunda mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi huo utakaofanyika Jumatatu ya Juni 1, 2026.

Jaji Mwambegele pia amewasisistiza  watendaji hao kuishi kwenye viapo vyao wakati wa utekelezaji majukumu yao ya Uchaguzi ili kujiepusha na upendeleo wa aina yoyote.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mafunzo hayo ya Makarani Waongozaji Wapiga Kura Vituoni Bw. Baraka Matonya amemuhakikishia Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwamba watafuata sheria, kanuni, miongozo na maelekezo ya Tume wakati wote wa Utekelezaji wa majukumu yao ya Uchaguzi .

Naye Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Isimani,Bi. Caroline Otieno amesema maandalizi ya uchaguzi  huo Mdogo wa Jimbo hilo, yamekamilika kwa asilimia 100 ambapo vifaa vyote vimepokelewa.

Uchaguzi huo utafanyika sambamba na uchaguzi mdogo katika kata 12 za Tanzania Bara ambazo ni Mzimuni iliyopo Manispaa ya Kinondoni; Zongomera, Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji wa Nzega; Ketare, Halmashauri ya Mji wa Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Nyingine ni kata ya Kala iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru; Bwongera, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Kibiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume.
Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa  Bi. Nuru Sovella akizungumza wakati wa mafunzo hayo. 
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Isimani,Bi. Caroline Otieno akizungumza na kusema kua maandalizi ya uchaguzi  huo Mdogo wa Jimbo hilo, yamekamilika kwa asilimia 100 ambapo vifaa vyote vimepokelewa.

Post a Comment

Previous Post Next Post