
Mkuu wa Idara ya Utamaduni, Makongamano na Utalii Taifa, Shujaa Daniel Kapaya, amewataka mashujaa wote nchini kutembelea makumbusho ya utamaduni na vivutio vya utalii wa kitamaduni vilivyopo kwenye maeneo yao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani.
Akitoa taarifa hiyo, Kapaya amesema kwa mujibu wa kalenda ya matukio ya kimataifa, Mei 18, 2026 ni Siku ya Makumbusho Duniani, ambapo idara hiyo kupitia sekta ya makongamano itajikita kuhamasisha wananchi kujifunza historia, mila na desturi za jamii mbalimbali nchini Tanzania pamoja na kukuza utalii wa ndani.
Amesema maadhimisho hayo yatatoa nafasi kwa wananchi kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na makumbusho kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu urithi wa taifa na umuhimu wa kuhifadhi utamaduni wa Mtanzania.
“Kwa mujibu wa taarifa hii, baadhi ya maeneo ya makumbusho yatafikiwa na wananchi pamoja na vikundi mbalimbali vya kijamii ili kujifunza mambo ya kale yanayohusu historia, mila na desturi,” amesema Kapaya.
Aidha, amesema mashujaa watakapopata fursa ya kutumia vyombo vya habari watashiriki pia kufanya midahalo na kutoa elimu kuhusu masuala ya mila na desturi pamoja na umuhimu wa utalii wa ndani katika kuchochea maendeleo ya taifa.
Kapaya amesema kauli mbiu ya Siku ya Makumbusho Duniani kwa mwaka 2026 ni; “Makumbusho Inaunganisha Dunia Iliyogawanyika” (Museum Unity a Divided World).
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment