" MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA AFISA HABARI BONIPHACE MAKENE MUSOMA

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA AFISA HABARI BONIPHACE MAKENE MUSOMA


Na Gabon Mariba - Musoma.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi,  ameshirikiana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Afisa Habari wa Ofisi ya Makamu wa Rais, marehemu Boniphace Makene, yaliyofanyika kijiji cha Mabui Melafuru, Kata ya Msanja, Wilaya ya Musoma mkoani Mara.Marehemu Boniphace Makene alifariki dunia tarehe 20 Aprili 2026 nchini Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu, taarifa iliyogusa mioyo ya wengi ndani na nje ya Serikali kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya habari na mawasiliano.Akizungumza wakati wa ibada na shughuli ya mazishi, Dkt. Nchimbi amesema taifa limepoteza mtumishi mwenye nidhamu, mchapakazi na aliyejituma kwa moyo wote katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.Amesema marehemu Makene alikuwa mtu wa ushauri mzuri, mwenye hekima na aliyekuwa msaada mkubwa katika Ofisi ya Makamu wa Rais, huku akisisitiza kuwa mchango wake utaendelea kukumbukwa na wengi waliopata nafasi ya kufanya kazi naye.Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.Aidha, Makamu wa Rais ametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu, akiwaomba kuwa na moyo wa subira na kuendelea kumuomba Mungu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.“Tutamkumbuka Boniphace Makene kwa uzalendo wake, bidii yake kazini na namna alivyowagusa watu wengi kupitia utumishi wake,” amesema Dkt. Nchimbi.@gabon_tza.#MisalabaMedia.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post