" MHANDISI BISHANGA ATIMIZA AGIZO LA RAIS SAMIA, FOLENI NA AJALI ZAANZA KUPUNGUA KWA KASI MKOANI MBEYA

MHANDISI BISHANGA ATIMIZA AGIZO LA RAIS SAMIA, FOLENI NA AJALI ZAANZA KUPUNGUA KWA KASI MKOANI MBEYA


Na Lydia Lugakila-Misalaba MediaMbeyaMeneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Suleiman Bishanga, amesema kuwa anaendelea kuhakikisha kunakuwa na usimamizi madhubuti wa matengenezo na marekebisho ya barabara zote mkoani humo ili kuhakikisha zinapitika kwa urahisi na usalama kwa watumiaji wa barabara, huku akisisitiza kuwa lengo ni kuondoa changamoto za usumbufu zilizokuwepo hapo awali zilizochangia ajali na msongamano.Mhandisi Bishanga amesema hayo Mei 15, 2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea na kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara katika Jiji la Mbeya.Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa madaraja, upanuzi wa barabara, ujenzi wa njia za michepuko pamoja na maboresho ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari ambayo yamekuwa yakisababisha ajali za mara kwa mara.Amesema kuwa yeye pamoja na timu yake wanaendelea kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha miundombinu hiyo inakuwa salama, imara na yenye kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.Mhandisi Bishanga pia amesema kuwa juhudi hizo zinaendana na maelekezo ya Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Mkoa wa Mbeya unaondokana na changamoto ya foleni, mikwamo ya magari pamoja na ajali zinazotokana na ubovu au uchache wa miundombinu ya barabara.“Mkoa wa Mbeya unaendelea kukua kwa kasi, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha barabara zinakuwa katika hali nzuri wakati wote ili kuondoa changamoto za usafiri na usafirishaji,” amesema Mhandisi Bishanga.Amewaomba wananchi kuwa wavumilivu wakati shughuli za ujenzi zikiendelea, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda miundombinu inayojengwa kwa gharama kubwa za Serikali ili iweze kudumu na kuwanufaisha wananchi kwa muda mrefu.Aidha, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo muhimu ambayo tayari imeanza kuleta matokeo chanya katika maeneo mbalimbali, ikiwemo eneo la Inyala ambapo awali magari yalikuwa yakikaa kwenye foleni kwa zaidi ya dakika 40 hadi saa mbili, hali ambayo sasa imeanza kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na maboresho yanayoendelea.Hata hivyo baadhi ya Wananchi wa Mbeya wameendelea kupongeza juhudi za Mhandisi Bishanga kwa usimamizi wake makini na wa karibu, wakisema kuwa miradi hiyo imeleta matumaini mapya katika sekta ya miundombinu na usafiri jijini humo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post